• HABARI MPYA

    Wednesday, May 18, 2016

    STARS MPYA, WATOTO WA KABUNDA, MGUNDA NDANI, YUMO PIA NA MJUKUU WA MAHADHI

    Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
    KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars Charles Boniface MKwasa ‘Master’ amemuita chipukizi Hassan Kabunda (pichani kushoto) katika kikosi kitakachomenyana na Kenya Mei 29 mjini Nairobi.
    Winga huyo wa Mwadui FC ya Shinyanga na mtoto wa beki wa zamani wa Yanga SC, Salum Kabunda ‘Ninja’ (sasa marehemu) amekuwa kivutio katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu huu.
    Mkwasa pia amemuita Jeremiah Juma wa Prisons ya Mbeya, mtoto wa mshambuliaji wa zamani wa Coastal Union ya Tanga, Juma Mgunda na Juma Mahadhi wa Coastal Union, mjukuu wa kipa wa zamani wa Simba, Omar Mahadhi ‘Bin Jabir’ (sasa marehemu).   
    Mkwasa pia amemrejesha kikosini kipa Deogratius Munishi ‘Dida’ na kumtema Ally Mustafa ‘Barthez’, wote wa Yanga.
    Kikosi kamili alichotaja leo Mkwasa kinaundwa na makipa; Deo Munishi ‘Dida’ (Yanga SC), Aishi Manula (Azam FC), Beno Kakolanya (Prisons FC).
    Mabeki; Nadir Haroub ‘Cannavaro’ (Yanga SC), Aggrey Morris (Azam FC), Erasto Nyoni (Azam FC), David Mwantika (Azam FC), Juma Abdul (Yanga SC), Mwinyi Hajji Mngwali (Yanga SC) na Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ (Simba SC).
    Viungo; Himid Mao (Azam Fc), Mohammed Ibrahim (Mtibwa Sugar), Shizza Kichuya (Mtibwa Sugar), Jonas Mkude (Simba SC), Ismail Issa Juma (JKT Ruvu), Mwinyi Kazimoto (Simba SC), Farid Mussa (Azam FC), Juma Mahadhi na Hassan Kabunda (Mwadui FC).
    Washambuliaji Thomas Ulimwengu (TP Mazembe – DRC), Mbwana Samatta (KRC Genk – Ubelgiji), Elias Maguri (Stand United), Ibrahim Hajib (Simba SC), John Bocco (Azam FC), Deus Kaseke (Yanga SC) na Jeremiah Juma (Prisons).
    Taifa Stars inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager, inatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki na Kenya, Harambee Stars Uwanja wa Kasarani mjini Nairobi, Kenya Mei, 29 mwaka huu.
    Mchezo ni sehemu ya maandalizi kwa timu zote mbili kujaindaa na michezo ya kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika mapema mwezi Juni, 2016.
    TFF kwa kushirikiana na FKF zimekubaliana kuwepo kwa mchezo huo wa kirafiki, utakotumika kama sehemu za maandalizi kwa timu zote kujiandaa na michezo ya kuwania kufuzu kwa AFCON 2017 mwezi Juni.
    Taifa Stars inatarajiwa kuingia kambini mapema Mei 22, mara baada ya kumalizika kwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kujiandaa na mchezo huo wa kirafiki kabla ya kuwakabili Misri katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Juni 4, mwaka huu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: STARS MPYA, WATOTO WA KABUNDA, MGUNDA NDANI, YUMO PIA NA MJUKUU WA MAHADHI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top