• HABARI MPYA

  Jumanne, Mei 24, 2016

  AL AHLY NA ZAMALEK ZATENGANISHWA MAKUNDI LIGI YA MABONGWA AFRIKA

  LIGI YA MABINGWA AFRIKA:
  Kundi A; Zesco United (Zambia), Al Ahly (Misri), Asec Mimosa (Ivory Coast) NA Waydad Casablanca ya Morocco
  Kundi B; Enyimba (Nigeria), Zamalek (Misri), ES Setif (Algeria) na Mamelodi Sundown (Afrika Kusini) 
  KOMBE LA SHIRIKISHO:
  KundiA; Yanga SC (Tanzania), TP Mazembe (DRC), MO Bejaia (Algeria) na Medeama (Ghana).
  Kundi B; Etoile du Sahel (Tunisia) Ahly Tripoli (Libya), FUS Rabat (Morocco) na Kawkab (Morocco).
  Al Ahly imepngwa kundi tofauti na wapinzani wao wa Misri, Zamalek katika Ligi ya Mabingwa Afrika

  VIGOGO wa Misri, Al Ahly na Zamalek wametenganishwa makundi katika Ligi ya Mabingwa Afrika.
  Katika droo iliyopangwa leo mjini Cairo, Misri, Ahly imepangwa Kundi A pamoja na Zesco United ya Zambia, Asec Mimosa ya Ivory Coast na Waydad Casablanca ya Morocco.
  Zamalek imepangwa Kundi B pamoja na Enyimba ya Nigeria, ES Setif ya Algeria na Mamelodi Sundown ya Afrika Kusini. 
  Kwenye Kombe la Shirikisho, Kundi linaundwa na Yanga SC ya Tanzania, TP Mazembe ya DRC, MO Bejaia ya Algeria na Medeama ya Ghana, wakati Kundi B linaundwa na timu za Kaskazini mwa Afrika tupu ambazo ni Etoile du Sahel ya Tunisia ambao ni mabingwa watetezi, Ahly Tripoli ya Libya, FUS Rabat na Kawkab zote za Morocco.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: AL AHLY NA ZAMALEK ZATENGANISHWA MAKUNDI LIGI YA MABONGWA AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top