• HABARI MPYA

  Jumatatu, Mei 23, 2016

  BARCELONA WAINUA NDOO YA MFALME HISPANIA, WAICHAPA SEVILLA 2-0 MADRID

  Wachezaji wa Barcelona na familia zao wakifurahia na faimlia zao taji la Kombe la Mfalme, maarufu kama Copa del Rey baada ya kuifunga Sevilla 2-0 katika mhezo wa fainali uliodumu kwa dakika 120 kufuatia dakika 90 kumalizika timu hizo zikiwa hazijafungana usiku wa kuamkia leo kwenye Uwanja wa Vicente Calderon mjini Madrid, Hispania. Mabao ya Barca Jordi Alba dakika ya 97 na Neymar dakika ya 120 na ushei. Katika mchezo uliokuwa mkali na wa kusisimua, Javier Mascherano wa Barcelona alitolewa kadi nyekundu dakika ya 36 kwa kumchezea rafu Kevin Gameiro akiwa anakwenda kufunga na Ever Banega wa Sevilla pia alitolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 90 na ushei kwa kumchezea rafu Neymar  PICHA ZAIDI GONGA HAPA
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: BARCELONA WAINUA NDOO YA MFALME HISPANIA, WAICHAPA SEVILLA 2-0 MADRID Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top