• HABARI MPYA

  Monday, May 30, 2016

  CAF YARUDISHA MTOANO KUANZIA ROBO FAINALI MICHUANO YA KLABU AFRIKA

  SHIRIKISHO la Soka Afrika limetaja mfumo mpya wa mashindano yake kuanzia mwakani, na sasa limerudisha mtindo wa mechi za mtoano kuanzia hatua ya Robo Fainali.
  katika kikao chake cha Jumanne ya Mei 24, mwaka 2016 mjini Cairo, Misri; Kamati ya Mashindano ya Klabu ya CAF ilikubaliana juu ya mfumo mpya wa Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho. 
  Mabadiliko katika mashindano hayo mawili yalitangazwa na Rais wa CAF, Issa Hayatou katika Mkutano Mkuu wa 38 wa shirikisho hilo uliofanyika mjini Mexico City, kwamba kuanzia mwakani kutakuwan na timu 16 katika hatua ya makundi.
  Baada ya raundi za awali, timu 32 zitafuzu kuwania hatua ya 16 Bora ya mashindano yote. 

  Watakaofuzu hatua ya 16 Bora kwa Ligi ya Mabingwa wataingizwa moja kwa moja katika makundi manne. baada ya mechi za makundi za nyumbani ugenini, washindi wawili wa juu wa kila kundi wataingia Robo Fainali ambayo itaanza kuchezwa kwa mtoano pia hadi fainali. 
  Klabu zitakazoongoza makundi zitaanzia ugenini katika Robo Fainali na kumalizia nyumbani.
  Katika Kombe la Shirikisho, timu 16 zitakazofuzu hatua ya makundi zitakuwa ni pamoja na zilizotolewa katika Ligi ya Mabingwa na baada ya hapo, mambo yatakwenda kama yalivyopangwa kwenye Ligi ya Mabingwa.
  CAF sasa ina tarehe 20 za kalenda ya mashindano hayo ambayo yataanza Marchi hadi Novemba kwa Ligi ya Mabingwa na hadi Desemba.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CAF YARUDISHA MTOANO KUANZIA ROBO FAINALI MICHUANO YA KLABU AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top