• HABARI MPYA

  Alhamisi, Mei 26, 2016

  WACHEZAJI 44 WAFUZU MAJARIBIO YA AWALI MBEYA CITY

  Na Doreen Favel, MBEYA
  ZOEZI kusaka nyota wapya (vijana) ambao wataingizwa kwenye timu  mbili za Mbeya City Fc U20 na ile ya wakubwa limefikia kwenye hatua nzuri hivi sasa baada ya wachezaji 44 kupatikana kwenye mchujo wa awali  uliolifanyika  leo ikiwa ni baada ya  siku nne   za mazoezi.
  Akizungumza baada ya kumalizika kwa mazoezi ya leo kwenye Uwanja wa Sokoine mjini hapa, Kocha Msaidizi wa City, Mohamed Kijuso amesema kuwa vijana 44 wamevuka mchujo wa kwanza na wataingia kwenye wamu ya pili inayotarajiwa kuanza.

  “Tulikuwa na kundi kubwa la wachezaji zaidi ya 106, baada ya mchujo leo, tumefanikiwa kupata  44 ambao wataingia kwenye awamu ya pili hapo kesho, lengo letu ni kuona tunapata walio bora kwa ajili ya timu yetu ya vijana na pia wachezaji saba ambao watakuwa tayari kucheza kwenye timu kubwa msimu ujao”, alisema. 
  Aidha, Kijuso amesema mchakato huo wa kusaka vipaji ambao ilikuwa ufikie tamati kesho, umesogezwa mbele mpaka hadi Jumamosi. "Wachezaji watakaopatikana kwenye mchujo wa kesho watapata nafasi ya kucheza mchezo mmoja wa kirafiki dhidi ya timu ya  Ilemi FC,"amesema.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: WACHEZAJI 44 WAFUZU MAJARIBIO YA AWALI MBEYA CITY Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top