• HABARI MPYA

  Jumatano, Mei 25, 2016

  FARID ANAANZA LEO MECHI NA YANGA, KIPRE TCHETCHE HAYUPO KABISA

  Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
  WINGA aliyefuzu majaribio katika klabu ya Deportivo Tenerife ya Daraja la Kwanza Hispania, Farid Mussa Malik anaanza leo katika kikosi cha timu yake Azam FC dhidi ya Yanga.
  Mchezo huo wa fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) unaanza Saa 10:30 jioni Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Mshambuliaji hatari wa Azam, Kipre Herman Tchetche raia wa Ivory Coast hayumo kabisa katika programu ya mchezo wa leo sawa na Mkenya, Allan Wanga. 
  Azam FC ambayo itaongozwa na kocha Msaidizi, Dennis Kitambi baada ya Muingereza Stewart Hall kung’atuka na kocha mpya, Mspanyola Zebensul Hernandez Roderiguez na Msaidizi wake, Jonas Garcia Luis kuwa bado hawajapatiwa vipaji vya kufanya kazi nchini.
  Farid Mussa Malik alipokuwa kwenye majaribio Hispania

  Upande wa Yanga nako, kocha Mholanzi, Hans van der Pluijm amepanga kikosi chake kamili cha ushindani, akiwaanzisha pamoja washambuliaji mzimbabwe Donald Dombo Ngoma na mrundi Amissi Joselyn Tambwe.  
  Vikosi vipo hivi; 
  Yanga SC; Deo Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Oscar Fanuel, Kevin Yondan, Vincent Bossou, Thaban Kamusoko, Simon Msuva, Haruna Niyonzima, Donald Ngoma, Amissi Tambwe na Deus Kaseke.
  Benchi; Ally Mustafa ‘Barthez’, Mwinyi Mngwali, Salum Telela, Nadir Haroub ‘Canavaro’, Matheo Anthony, Mbuyu Twite na Geofrey Furaha Mwashiuya.
  Azam FC; Aishi Manula, Erasto Nyoni, Gadiel Michael, Aggrey Morris, Abdallah Kheri, Jean Baptiste Mugiraneza, Himid Mao, Mudathir Yahya, John Bocco, Ramadhani Singano ‘Messi’ na Farid Mussa.
  Benchi; Mwadini Ali, Said Mourad, Frank Domayo, Kipre Bolou, Didier Kavumbagu, Ame Ally na Shaaban Idd.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: FARID ANAANZA LEO MECHI NA YANGA, KIPRE TCHETCHE HAYUPO KABISA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top