• HABARI MPYA

  Saturday, May 28, 2016

  ZIDANE: RONALDO ATACHEZA NA MAUMIVU YAKE LEO

  KOCHA Zinedine Zidane amesema nyota wake, Cristiano Ronaldo yuko fiti kwa asilimia 100 kwa ajili ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, lakini amekiri Mreno huyo atalazimika kucheza na maumivu ili kumaliza mechi hiyo.
  Mfaransa huy na mchezaji wa zamani wa Real Madrid amesema hakuna wasiwasi Ronaldo ataanza dhidi ya mahasimu wao, Atletico Madrid na anatarajia atamalaiza mechi.
  Ronaldo aliumia Jumanne baada ya kugongana na Kiko Casilla kwenye mazoezi na akalazimika kutoka nje kutubiwa na nesi mguu wake.
  Cristiano Ronaldo amesahau maumivu yake na kujifua kikamilifu kwa ajili ya fainali leo PICHA ZAIDI GONGA HAPA 


  Zidane alisema maneno kama hayo kabla ya mchezo wa Nusu Fainali ya michuano hiyo dhidi ya Manchester City Uwanja wa Etihad mwezi April, baada ya Ronaldo kuumia nyama. Lakini Mfaransa huyo alisistiza jana: 
  "Si kitu kile kile. Alikuwa anasikia maumivu makali, lakini kwa sasa yupo fiti kwa asilimia 100, na zaidi ya hayo anacheza fainali. 
  "Unapocheza fainali kama unasikia maumivu yoyote, unajipa ujasiri wa kuahau. Alikuwa anasikia maumivu kidogo, lakini si kitu na kesho (leo) atakuwa fiti kwa asilimia 100," amesema.
  Sergio Ramos, aliyefunga bao la kusawazisha dakika ya tatu ya muda wa nyongeza katika fainali ya mwisho timu hizo kukutana miaka miwili iliyopita ikishinda kwenye muda wa nyongeza, amesema atajituma kurudia matokeo hayo.
  Ramos, ambaye pamoja na wachezaji wenzake, alipigwa picha akiwa na nyota wa Hollywood, Richard Gere na mpenzi wake, Alejandra Silva, na akasema: "Tumepambana mno ili kufika fainali na tuko hatua moja kufika kileleni. Tunakwenea kuacha ngozi zetu uwanjani ili kupata taji,".
  Wasanii wa Italia, Andrea Bocelli na nyota wa muziki Alicia Keys watatumbuiza kabla ya fainali hiyo Uwanja wa San Sito mjini Milan, Italia usiku wa leo.
  Mwigizaji Gere mwenye umri wa miaka 66, na Silva mwenye umri wa miaka 33 walikuwepo kwenye mazoezi ya Real jana na leo watawasapoti vigogo hao wa Hispania.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ZIDANE: RONALDO ATACHEZA NA MAUMIVU YAKE LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top