• HABARI MPYA

  Ijumaa, Mei 27, 2016

  MAN UNITED KUMPA MOURINHO PAUNI MILIONI 200 ASAJILI WAKALI WAPYA

  Jose Mourinho anatarajiwa kutajwa rasmi leo kuwa kocha mpya wa Manchester United  PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  RATIBA YA ZIARA YA KUJIANDAA NA MSIMU MAN UNITED 

  Julai 22 ‒ Borussia Dortmund, Uwanja wa Shanghai, Kombe la Kimataifa
  Julai 25 ‒ Manchester City, Uwanja wa Kimataifa wa Beijing, Kombe la Kimataifa
  Agosti 7 ‒ Leicester City, Wembley, Ngao ya Jamii
  Msimu mpya wa Ligi Kuu ya England utaanza Agosti 13
  MANCHESTER United itampa Jose Mourinho Pauni Milioni 200 kusajili wachezaji wapya na wadhamini wa kocha huyo Mreno wametangaza rasmi kwamba sahiba wao huyo anakwenda Manchester.
  Mourinho alionekana akirejea nyumbani kwake London amevalia suti kali ya Hugo Boss baada ya kukamilisha mipango ya kuhamia Manchester United.
  Kampuni ya Bizarrely, Jaguar — moja ya wadhamini wa Mourinho wametangaza kabla ya klabu hiyo kwamba Jose anahamia United.
  United itamtangaza rasmi Mourinho kuwa kocha wao mpya leo na mara moja ataanza kazi ya kusajili kikosi cha msimu ujao.
  Kocha huyo wa zamani wa Chelsea atasaini Mkataba wa miaka mitatu wenye thamani ya Pauni Milioni 45 na atapewa bajeti ya Pauni Milioni 200 kwa ajili ya usajili wa kikosi cha msimu ujao.
  Mourinho mwenye umri wa miaka 53 tayari ameeleza maeneo katika kikosi cha United, ambayo anafikiri anahitaji kuyaboresha baada ya kikao chake na Makamu Mwenyekiti Mtendaji, Ed Woodward.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MAN UNITED KUMPA MOURINHO PAUNI MILIONI 200 ASAJILI WAKALI WAPYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top