• HABARI MPYA

    Thursday, May 26, 2016

    TFF YAUTEKA UCHAGUZI WA YANGA, YAANZA KUGAWA FOMU ZA WAGOMBEA KARUME

    KAMATI ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), imetangaza leo Mei 27, 2016 kuanza kwa mchakato wa kuchukua fomu za kugombea uongozi katika Klabu ya Young Africans ya Dar es Salaam inayotarajia kufanya uchaguzi tarehe 25 Juni mwaka huu.
    Nafasi zinazogombewa ni pamoja na nafasi ya Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na wajumbe wanane wa Kamati ya Utendaji.
    Makao makuu ya Yanga, eneo la Jangwani, Dar es Salaam

    Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, Aloyce Komba fomu zinapatikana katika ofisi za TFF zilizoko Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Ilala jijini Dar es Salaam. Vilevile utaratibu unafanyika ili fomu ziweze kupatikana katika tovuti ya shirikisho www.tff.or.tz
    Fomu zinapatikana kwa gharama ya Sh 200,000 kwa nafasi ya mwenyekiti na makamu mwenyekiti na Sh 100,000 kwa wagombea wa nafasi ya ujumbe wa kamati ya utendaji. Mwisho wa kuchukua fomu ni tarehe 31 Mei, 2016.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TFF YAUTEKA UCHAGUZI WA YANGA, YAANZA KUGAWA FOMU ZA WAGOMBEA KARUME Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top