• HABARI MPYA

  Jumatatu, Mei 23, 2016

  AZAM YAANDAA MICHUANO YA VIJANA AFRIKA MASHARIKI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, imeonyesha kweli imedhamiria kuinua soka la vijana nchini baada ya leo kutangaza kuandaa michuano ya vijana ya Afrika Mashariki itakayoanza kutimua vumbi kwenye viunga vya Azam Complex Juni Mosi hadi Juni 5 mwaka huu.
  Kwa kuanzia mwaka huu michuano hiyo itakayojulikana kama ‘Azam Youth Cup 2016’ itahusisha timu nne pekee, za Tanzania zikiwa ni kikosi cha vijana ya Azam FC ‘Azam Academy’ na Future Stars Academy (Arusha) pamoja na timu mbili nje ya Tanzania  Ligi Ndogo Academy (Kenya) na Football for Good Academy (Uganda).
  Mwenyekiti wa Azam FC, Sheikh Said Mohammed (katikati) akizungumza na Waandishi wa Habari leo

  Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari leo, Mwenyekiti wa Azam FC, Said Mohamed, alisema kuwa malengo makubwa ya michuano hiyo ni kukuza vipaji vya vijana na baadaye kupata wachezaji watakaocheza katika timu kubwa ya Azam FC ambao ndio watakuza soka.
  “Moja ya madhumuni ya kuanzisha Azam FC ni kukuza soka la vijana, kwa hiyo kwa kusisitiza hilo leo tunatangaza kuandaa michuano ya vijana ya Afrika Mashariki, kutakuwa na timu kutoka Kenya, Uganda na Tanzania, wenzetu wote duniani waliopata maendeleo walianza chini huku kwa vijana na wakapanda juu, hawakuanza juu ndio wakashuka chini.
  “Hivyo kuwa na timu kubwa pekee hakutoshi lazima uwe na timu za vijana ili hao vijana ndio wawe chemchem ya kuweza kupatikana maendeleo ya mpira,” alisema.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: AZAM YAANDAA MICHUANO YA VIJANA AFRIKA MASHARIKI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top