• HABARI MPYA

  Wednesday, May 25, 2016

  MOURINHO AMSHUSHA IBRAHIMOVIC OLD TRAFFORD, ALETA NA BEKI LA EVERTON PIA

  Zlatan Ibrahimovic (kulia) akiwasili Uwanja wa mazoezi wa Sweden mjini Stockholm kujiandaa na Euro 2016 nchini Ufaransa  PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  IBRAHIMOVIC'S SCORING RECORD

  Malmo: 47 appearances, 18 goals
  Ajax: 110 apps, 48 goals
  Juventus: 92 apps, 26 goals
  Inter Milan: 117 apps, 66 goals
  Barcelona: 46 apps, 22 goals
  AC Milan: 85 apps, 56 goals
  PSG: 180 apps, 156 goals 
  MRENO Jose Mourinho will atatajwa kuwa kocha mpya wa Manchester United ndani ya saa 48 zijazo na anatarajiwa kumsajili mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic awe mchezaji wake wa kwanza kumteremsha Old Trafford.
  Ibrahimovic yuko huru baada ya kuondoka Paris Saint-Germain, lakini bado zinahitaji Pauni Milioni 8 za kusaini Mkataba wa zaidi ya miaka miwili na mshahara wa zaidi ya Pauni 200,000 kwa wiki.
  Mkongwe huyo wa kimataifa wa Sweden mwenye umri wa miaka 34, ni miongoni mwa nyota wanaaotakiwa sana na Mtendaji Mkuu wa Man United, Ed Woodward katika zama mpya za Mourinho, lakini inaaminika pia anapenda kurejea klabu yake ya zamani, Inter Milan.
  Uteuzi wa Mourinho umekaribia kutimia baada ya wakala wake, Jorge Mendes kukutana na Woodward mjini London jana na kukubaliana Mkataba wa miaka mitatu wenye thamani ya Pauni Milioni 45 na kujadili usajili wa wachezaji. 
  Miongoni mwa wachezaji anaotarajiwa kuwasajili Mourinho ni pamoja na beki wa Everton, John Stones, ambaye alijaribu kumsajili alipokuwa Chelsea msimu uliopita. 
  Mourinho atakutana tena na upinzani wa mpinzani wake wa zamani walipokuwa Hispania, Pep Guardiola ambaye naye anahamia Manchester City.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MOURINHO AMSHUSHA IBRAHIMOVIC OLD TRAFFORD, ALETA NA BEKI LA EVERTON PIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top