• HABARI MPYA

  Jumatatu, Mei 30, 2016

  MASHABIKI WAPIGANA HADI DAMU UWANJA WA WEMBLEY

  MASHABIKI wa Barnsley walilazimika kukimbia kukwepa kikundi cha mashabiki wa Millwall waliowavamia kuwashambulia Jumapili Uwanja w aWembley, London.
  Mashabiki wa Millwall walipatwa hasira baada ya timu yao kuruhusu bao la tatu wakifungwa 3-1 katika fainali ya mchujo wa League One England na kundi moja likawavamia upande wa mashabiki wa Barnsley. 
  Wachache waliweza kufanya licha ya vizuizi vya Polisi na walkipambana nao kabla ya uvamizizi huo. 
  Shabiki wa Millwall akimshindilia ngumi kichwani shabiki wa Barnsley  PICHA ZAIDI GOGA HAPA   

  Mashabiki wa Barnsley baadhi yao wakiwa na familia zao walilazimika kukimbia kuwakwepa wavamizi, lakini vurugu zikawa kubwa na mashabiki wa Millwall walinaswa na kamera wakiwashindilia ngumu wenzao na kuwajeruhi hadi baadhi yao kutokwa damu.
  Chama cha Soka England (FA) kimelaani vizuru hizo na kimesema kitafanya uchunguzi wa kina ili kuwabaini wahusika wachukuliwe hatua
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MASHABIKI WAPIGANA HADI DAMU UWANJA WA WEMBLEY Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top