• HABARI MPYA

  Jumatatu, Mei 30, 2016

  MOURINHO AMTAKA RIO FERDINAND AWE MSAIDIZI WAKE MAN UNITED, GIGGS...

  KOCHA Jose Mourinho amemuorodhesha Rio Ferdinand katika orodha ya watu anaotaka kufanya nao kazi kwenye benchi la Ufundi katika mapinduzi yake Manchester United.
  Mreno alitangazwa kumrithi Mholanzi Louis van Gaal Ijumaa akienda na masahiba zake anaaowaamini Rui Faria na Silvino Louro katika zama mpya Old Trafford.
  Mourinho anataka Ferdinand awe mmoja wa makocha wake Wasaidizi katika benchi imara la Ufundi Man United.
  Jose Mourinho anamtaka Rio Ferdinand (kulia) akiwa na gwiji mwenzake wa Old Trafford, Ryan Giggs (kushoto) awe mmoja wa makocha wake Wasaidizi Manchester United PICHA ZAIDI GONGA HAPA   

  WASIFU WA RIO FERDINAND MAN UNITED 

  Jumla ya mechi: 444
  Mabao aliyofunga: 8
  Mataji aliyotwaa: 
  Ligi Kuu (6): 2002–03, 2006–07, 2007–08, 2008–09, 2010–11, 2012–13
  Kombe la Ligi (3): 2005–06, 2008–09, 2009–10
  Ngao ya Jamii (6): 2003, 2007, 2008, 2010, 2011, 2013
  Ligi ya Mabingwa Ulaya (1): 2007–08
  Klabu Bingwa ya Dunia ya FIFA  (1): 2008
  Kuna wasiwasi juu ya mustakabali wa Ryan Giggs, ambaye anatarajiwa kuwa na mazungumzo na bosi wake mpya akirejea kutoka mapumzikoni Dubai.
  Mourinho anaelekea kutaka kuwabakiza watu ambao wanaijua vizuri Man United na ni matumaini Giggs ataendelea na kazi yake hiyo ya muda mrefu sasa, ambayo ni daraja kati ya timu ya vijana ya 21 na kikosi cha kwanza.
  Hiyo inatarajiwa pia kwa Ferdinand, ambaye ameitumikia klabu hiyo kwa miaka 12 akishinda mataji sita ya Ligi Kuu ya England na Ligi ya Mabingwa Ulaya=.
  Ferdinand, ambaye anaendelea na masomo ya ukocha kwa sasa, atakuwa na maamuzi atakapopelekewa ofa ya kufundisha United kuikubali au kuamua kutulia familia yake changa nyumbani kwaje, Kusini Mashariki
  Rio ana watoto watatu alioachiwa na mkewe, Rebecca aliyefariki kwa ugonjwa wa kansa mwaka jana.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MOURINHO AMTAKA RIO FERDINAND AWE MSAIDIZI WAKE MAN UNITED, GIGGS... Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top