• HABARI MPYA

  Jumatatu, Mei 23, 2016

  SERENGETI BOYS YALIKOSAKOSA KOMBE LA INDIA, KUWANIA NAFASI YA TATU NA MALAYSIA

  Na Mwandishi Wetu, GOA
  TANZANIA leo imetupwa nje ya mchuano wa kuwania ubingwa wa mashindano ya vijana chini ya umri wa miaka 16 ya Shirikisho la Soka India (AIFF Youth Cup 2016 U-16) mjini hapa.
  Serengeti Boys imeaga baada ya Korea Kusini leo kutoa sare ya 0-0  na India katika mchezo wake wa mwisho Uwanja wa Tilak Maidan mjini hapa.
  Kwa matokeo hayo, Korea inamaliza nafasi ya pili nyuma ya Marekani na kufuzu fainali ambako itamenyana na mshindi huyo wa kwanza Jumatano.

  Korea imeizidi Tanzania kwa wastani wa mabao tu, baada ya zote kulingana kwa pointi, sita kila moja, wakati Marekani imemaliza na pointi nane baada ya leo kuifunga Malaysia 2-1. 
  Sasa Tanzania itamenyana na tena Malaysia Jumatano kuwania nafasi ya tatu baada ya mchezo wa hatua ya awali timu hizo kutoa sare ya 2-2 juzi.
  Mechi nyingine, Tanzania ilitoa sare ya 1-1 na Marekani kabla ya kuwafunga wenyeji, India 3-1. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SERENGETI BOYS YALIKOSAKOSA KOMBE LA INDIA, KUWANIA NAFASI YA TATU NA MALAYSIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top