• HABARI MPYA

  Alhamisi, Mei 26, 2016

  WAGHANA WAIHOFIA YANGA, BOSI WAO ASEMA LITAKUWA 'MECHI LA KUFA MTU'

  TIMU ye Medeama ya Ghana imesema itakuwa shughuli pevu kukutana Yanga SC ya Tanzania katika hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, kwa sababu sasa inafundishwa na kocha wao wa zamani, Mholanzi Hans van der Pluijm.
  Mtendaji Mkuu wa Medeama, James Essilfie amesema hayo jana baada ya kupangwa droo ya makundi ya Kombe la Shirikisho, wao wakiangukia Kundi A pamoja na Yanga, TP Mazembe ya DRC na Mo Bejaia ya Algeria.
  "Yanga inafundishwa na Hans Van der Pluijm, kocha wa zamani wa Medeama na kucheza nao itakuwa mechi nzuri,"amesema Essilfie na kuongeza;
  "Tumefurahishwa na makundi, timu nyingine katika kundi zitasaidia kuonyesha ubora wa Medeama. Wengi walitilia shaka uwezo wetu tulipopangiwa Mamelodi Sundaowns (ya Afrika Kusini) katika hatua ya mchujo, lakini tumethibitisha ubora wetu," amesema Essilfie ambaye timu yake iliitoa Mamelodi na kuingia kwenye makundi.
  Medeama nayo inavaa jezi za kijani na njano kama Yanga
  Ameongeza; "Kundi hili litatuhamaisha na nina uhakika tutafika mbali. TP Mazembe haitishi kama ilivyokuwa kabla. Wakati tumekuwa tukifanya vizuri dhidi ya timu za kiwango cha juu. MO Bejaia imewatoa mabingwa wa Ghana, Ashantigold, na tunatumai tutawalipia kisasi,". 
  Medeama imepangwa Kundi A katika Kombe la Shirikisho Afrika pamoja na mabingwa wa zamani barani, TP Mazembe ya DRC, MO Bejaia ya Algeria na Yanga ya Tanzania.
  Kundi B linaundwa na timu za Kaskazini mwa Afrika tupu ambazo ni Etoile du Sahel ya Tunisia ambao ni mabingwa watetezi, Ahly Tripoli ya Libya, FUS Rabat na Kawkab zote za Morocco.
  Medeama wataanzia ugenini kwa TP Mazembe mjini Lubumashi Juni 17, siku ambayo Yanga itakuwa ugenini kwa MO Bejaia nchini Algeria Juni 17.

  Ikitoka Lubumbashi itamenyana na MO Bejaia kabla ya kuifuata Yanga Julai 15 mjini Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: WAGHANA WAIHOFIA YANGA, BOSI WAO ASEMA LITAKUWA 'MECHI LA KUFA MTU' Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top