• HABARI MPYA

  Jumamosi, Mei 28, 2016

  NIYONZIMA ALIPOKUTANA NA MKALI WA YANGA YA 1998 LIGI YA MABINGWA, BANZA TSHIKALA

  Kiungo wa Yanga SC, Haruna Niyonzima raia wa Rwanda (kulia) akiwa na kiungo wa zamani wa timu hiyo, Banza Tshikala aliyewika kati ya mwaka 1997 na 2000 baada ya kukutana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Jumatano baada ya fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC), timu hiyo ikishinda 3-1 dhidi ya Azam FC. Banza alikuwemo kwenye kikosi kilichoipa Yanga tiketi ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 1998 akicheza kama kiungo mkabaji na beki wa kati wakati mwingine. Niyonzima naye mwaka huu ameiwezesha Yanga kufuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: NIYONZIMA ALIPOKUTANA NA MKALI WA YANGA YA 1998 LIGI YA MABINGWA, BANZA TSHIKALA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top