• HABARI MPYA

  Alhamisi, Mei 26, 2016

  MAN UNITED WATAKA KUSAJILI MIDO KIRAKA LA ATLETICO MADRID

  KLABU ya Manchester United inataka kumsajili mchezaji mwenye thamani ya Pauni Milioni 54, Saul Niguez wa Atletico Madrid, ikiwa ni sehemu ya mipango ya kocha mpya mtarajiwa, Jose Mourinho.
  Saul ni moja ya bidhaa adimu kwa sasa Hispania na bao lake pekee dhidi ya Bayern Munich katika mchezo wa kwanza wa Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya limezidi kumpadisha chati.
  Kinda huyo wa umri wa miaka 21, yuko sawa na Renato Sanches, ambaye Man United walijaribu kumsajili akiwa Benfica kabla ya kuzidiwa kete na Bayern.

  Kiungo wa Atletico Madrid, Saul Niguez anatakiwa Manchester United ya msimu ujao  PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  Saul amecheza mashindano yote akiwa na Atletico kwa misimu miwili iliyopita na kutokea kuwa tegemeo la kocha Diego Simeone katika kikosi chake cha kwanza.
  Anaweza kucheza kama kiungo kati au wa pembeni — ana uhakika wa kupata namba mbele ya Mourinho. Wakati akicheza kwa mkopo Rayo Vallecano msimu wa 2013-14, Saul alicheza pia kama beki wa kati.
  Hajawahi kuchezea kikosi cha Hispania cha wakubwa, lakini
  Saul amechezea mechi 47 vikosi vya timu za vijana za nchi hiyo.
  Kwa mara ya kwanza aliitwa kikosi cha wakubwa mwaka jana kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Costa Rica na wa kufuzu Euro 2016 dhidi ya Belarus, lakininhakukanyaga uwanjani kwenye mechi. 
  Pamoja na hayo, kocha wa Hispania, Vicente del Bosque amemjumuisha kwenye kikosi cha mwisho cha wachezaji 23 kitakachokwenda kwenye michuano ya Euro 2016 nchini Ufaransa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MAN UNITED WATAKA KUSAJILI MIDO KIRAKA LA ATLETICO MADRID Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top