• HABARI MPYA

  Friday, May 27, 2016

  KCCA MABINGWA WA LIGI YA AZAM UGANDA

  TIMU ya Mamlaka ya Jiji la Kampala (KCCA) imefanikiwa kutwaa taji la 11 la Ligi Kuu ya Azam Uganda baada ya kuipiku Vipers katika siku ya kufunga pazia la msimu 2015/16 leo.
  KCCA imetoa sare ya 1-1 na Sadolin Pints Uwanja wa Nakivubo na hivyo kumaliza na pointi 29 baada ya mechi 15, ikiizidi kwa pointi moja, Vipers ambayo nayo imetoa sare ya 1-1 leo na The Saints Uwanja wa Mandela, Namboole.
  Fred Ssegujja almanusra awakoseshe taji mabingwa hao baada ya kutangulia kuwafungia Sadolin, lakini Joseph Ochaya akawasawazishia KCCA.
  SC Villa imeifunga Maroons 4-1 Uwanja wa Luzira, lakini walikuwa ni URA waliiobuka na ushindi mnono zaidi baada ya kuifunga SC Victoria University iliyoshuka daraja mabao 6-1 Uwanja wa Mehta, Lugazi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KCCA MABINGWA WA LIGI YA AZAM UGANDA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top