• HABARI MPYA

  Jumatatu, Mei 23, 2016

  HATIMAYE MAN UNITED YAMFUKUZA VAN GAAL

  HATIMAYE Manchester United imemfukuza kocha Mholanzi Louis van Gaal siku mbili baada ya kuiwezesha timu hiyo kutwaa Kombe la FA ikiifunga 2-1 Crystal Palace katika fainali.
  Mholanzi huyo anafukuzwa baada ya matokeo mabaya katika Ligi Kuu ya England na nafasi yake itachukuliwa na kocha wa zamani wa Chelsea, Inter Milan na Real Madrid, Jose Mourinho.
  Wote aliokuwa anafanya nao kazi katika benchi la Ufundi, Van Gaal United akiwemo kocha Msaidizi, Albert Stuivenberg na kocha wa makip, Frans Hoek - nao pia wametimuliwa.  

  Louis van Gaal (kulia) amefukuzwa Man United na Jose Mourinho (kushoto) anachukua nafasi yake  

  Ed Woodward aliwasili katika Uwanja wa mazoezi wa Manchester United, Carrington kwa ajili ya mazungumzo na Van Gaal mapema leo.
  Mwenyekiti huyo Mtendaji akamueleza Van Gaal hataendelea kuifundisha klabu hiyo na wanatarajia kumchukua Mourinho badala yake.
  Van Gaal aliwasili Carrington majira ya Saa 2.45 asubuhi ya leo pamoja na wawaidizi wake katika benchi la Ufundi.
  Mourinho anatarajiwa kuwa na mazungumzo zaidi na United kesho na kuna uwezekano akasaini Mkataba wa miaka mitatu pamoja na Rui Faria na Silvino Louro, kocha wa makipa atakaokuwa nao katika benchi la Ufundi.
  Mustakabali wa Ryan Giggs Man United sasa upo kwa Mourinho, ambaye anatarajiwa kumbakiza gwiji huyo wa klabu, nyota wa zamani wa Wales. 
  Van Gaal aliingia Man United miaka miwili iliyopita, akirithi mikoba ya David Moyes aliyekuwa kocha wa kwanza baada ya kustaafu kwa Sir Alex Ferguson na anafukuzwa akiwa amebakiza msimu mmoja katika Mkataba wake.
  Mourinho amekuwa nje ya kazi tangu afukuzwe Chelsea kwa matokeo mabaya pia Desemba mwaka jana.
  Chini ya Van Gaal, United ilipoteza asili yake ya soka ya kushambulia ikifunga mabao 49 katika tu Ligi Kuu ya England msimu huu, ambayo ni machache mno kwa miaka 26 - na pia imekosa nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya wakizidiwa kete na mahasimu wao, Manchester City kwa tofauti ya mabao.
  Taji la kwanza la Kombe la FA tangu mwaka 2004 lilitarajiwa kumbakiza Van Gaal United, lakini Nahodha Wayne Rooney alisema kwamba hawakuwa katika ubora pamoja na kutwaa taji hilo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: HATIMAYE MAN UNITED YAMFUKUZA VAN GAAL Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top