• HABARI MPYA

  Jumanne, Mei 31, 2016

  'RAMBO' THOM ULIMWENGU AINGIA KAMBINI STARS MAANDALIZI NA MISRI

  Ulimwengu amejiunga na kambi ya Taifa Stars
  Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
  NYOTA wa kimataifa wa Tanzania, Thomas Emmanuel Ulimwengu amejiunga na timu ya taifa, Taifa Stars leo kwa ajili ya mchezo wa kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika dhidi ya Misri Jumamosi wiki hii Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Dar es Salaam.
  Ulimwengu 'Rambo' amechelewa kujiunga na Taifa Stars kutokana na klabu yake, TP Mazembe ya DRC kumuomba abaki kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya nchi hiyo dhidi ya mahasimu, AS Vita.
  Na usiku wa kuamia leo, Ulimwengu alitua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam na moja kwa moja kuingia kambini Stars.
  Taifa Stars inayodhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager ili kukamilika, sasa inamsubiri mshambuliaji na Nahodha, Mbwana Samatta wa KRC Genk ya Ubelgiji pekee, ambaye naye klabu yake ilimuomba abaki kwa ajili ya mchezo wa mwisho wa mchujo wa kuwania kucheza Europa League msimu ujao.
  Samatta na Ulimwengu, wote wameziongoza klabu zao kushinda mwishoni mwa wiki, Genk ikiilaza 5-1 Sporting Charleroi  na kufuzu Europa League na Mazembe ikiichapa 2-0 AS Vita katika Ligi ya DRC. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: 'RAMBO' THOM ULIMWENGU AINGIA KAMBINI STARS MAANDALIZI NA MISRI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top