• HABARI MPYA

  Tuesday, May 31, 2016

  HANS POPPE: HAJAACHWA JUUKO WALA KIIZA, WA KIGENI WOTE BADO WACHEZAJI WA SIMBA

  Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
  MWENYEKITI wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amesema kwamba hakuna mchezaji wa kigeni aliyeachwa hadi sasa na kwamba vyombo vya habari vimekuwa vikiripoti tofauti.
  Akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE jana, Hans Poppe amesema kwamba walikuwa wakilalamikia uwajibikaji usioridhisha wa wachezaji wa kigeni wa klabu hiyo, lakini hawakusema wanaachwa.
  “Ni kiongozi gani wa Simba alitamka mchezaji fulani kaachwa Simba? Hakuna, hayo ni maneno ya magazeti tu. Sisi tulililalamikia uwajibikaji usioridhisha wa wachezaji wa kigeni, hatujawaachaa,”alisema.
  Zacharia Hans Poppe amesema kwamba hajaachwa mchezaji yeyote wa kigeni Simba

  Hans Poppe amesema kwamba wachezaji wote wenye mikataba na Simba wanaendelea kupewa stahiki zao kama kawaida wakiwemo hao wa kigeni.
  Mwishoni mwa msimu, Simba SC ilitofautiana na wachezaji wake wa kigeni baada ya kugoma kwenda Songea kucheza mechi ya pili kuelekea mwishoni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Majimaji.
  Wachezaji hao ni kipa Vincent Angban kutoka Ivory Coast, mabeki Emery Nimubona kutoka Burundi, Juuko Murshid, kiungo Brian Majwega, mshambuliaji Hamisi Kiiza wote kutoka Uganda na kiungo Justice Majabvi kutoka Zimbabwe ambao waligoma kwa kucheleweshewa kwa wiki moja mishahara ya Aprili.  
  Hata hivyo, hivyo Simba SC iliwalipa mishahara yao wachezaji hao na kuteua wawili, Angban na Majabvi kwenda Songea siku moja kabla ya mechi.
  Kilichofuatia hapo ni habari za magazeti kwamba Simba SC itaacha wachezaji wote wa kigeni na kusajili wapya.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: HANS POPPE: HAJAACHWA JUUKO WALA KIIZA, WA KIGENI WOTE BADO WACHEZAJI WA SIMBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top