• HABARI MPYA

  Jumanne, Mei 31, 2016

  RASHFORD APEWA 'SITI' KIKOSI CHA MWISHO ENGLAND EURO 2016

  KOCHA Roy Hodgson ametaja kikosi cha wachezaji 23 kwa ajili ya fainali za Euro 2016 akimjumuisha Marcus Rashford pamoja na Daniel Sturridge wakati Danny Drinkwater na Andros Townsend wametemwa sambamba na majeruhi, Fabian Delph.
  Rashford alifanya vizuri katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa Ijumaa, dhidi ya Australia akifunga bao baada ya sekunde 138, wakati Sturridge amedhihirisha kiasi cha kutosha kwamba yuko fiti. 
  Mshindi wa taji la Ligi Kuu ya England, Drinkwater, Townsend wa Newcastle na kiungo wa Manchester City, Delph wanakosekana kwenye kikosi cha michuano baada ya kupunguzwa kutoka wachezaji 26 hadi 23.
  Mshambuliaji wa Manchester United, Marcus Rashford amejumuishwa kwenye kikosi cha Roy Hodgson cha wachezaji 23 timu ya taifa ya England PICHA ZAIDI GONGA HAPA    

  KIKOSI KAMILI CHA ENGLAND KWA NAMBA ZAO EURO 2016 

  1. Joe Hart, 2. Kyle Walker, 3. Danny Rose, 4. James Milner
  5. Gary Cahill, 6. Chris Smalling, 7. Raheem Sterling, 
  8. Adam Lallana, 9. Harry Kane, 10. Wayne Rooney,
  11. Jamie Vardy, 12. Nathaniel Clyne,13. Fraser Forster,
  14. Jordan Henderson,15. Daniel Sturridge,16. John Stones
  17. Eric Dier,18. Jack Wilshere,19. Ross Barkley, 
  20. Dele Alli, 21. Ryan Bertrand, 22. Marcus Rashford na 
  23. Tom Heaton.


  Hiki kitakuwa kikosi cha kwanza cha Hodgson kwa mchezo na Urusi? 
  GK: Hart; RB:Walker, CB: Smalling, CB: Cahill, LB: Rose; DCM: Milner, M: Lallana, M: Sterling, ACM: Rooney; F: Kane, F: Vardy 
  England itamenyana na Ureno Uwanja wa Wembley Alhaamisi kabla ya kwenda Ufaransa ambako wataanza na Urusi Juni 11 mjini Marseilles. 
  Uamuzi wa Hodgson unamaanisha England itakuwa na makipa watatu, mabaeki saba, viungo wanane na washambuliaji watano Ufaransa katika kikosi kinachomjumuisha kinda anayeinukia vizuri, Rashford.
  Kiasi cha miezi mitatu baada ya kucheza mechi ya kwanza kikosi cha kwanza cha Man United tangu alipopandishwa, kinda huyo wa umri wa miaka 18 ameshinda Kombe la FA na kusainishwa Mkataba mpya kabla ya kuchukuliwa kikosi cha Euro 2016.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: RASHFORD APEWA 'SITI' KIKOSI CHA MWISHO ENGLAND EURO 2016 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top