• HABARI MPYA

  Jumanne, Mei 24, 2016

  AS VITA YAENGULIWA LIGI YA MABINGWA KWA KUTUMIA ALIYEFUNGIWA

  KAMATI ya Maandalizi ya michuano ya klabu ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) leo imeiondoa AS Vita ya DRC kwenye hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kosa la kumtumia mchezaji Idrissa Traore katika hatua za awali akiwa anatumikia adhabu.
  Kamati hiyo imefikia uamuzi huo katika kikao chake mjini Cairo, Misri yalipo makao makuu ya CAF baada ya kupitia malalamiko ya klabu ya Stade Malien ya Mali dhidi ya As Vita juu ya Idrissa Traore.

  AS Vita imeondolewa michuano ya Ligi ya Mabingwa kwa kumtumia Idrissa Traore akiwa anatumia adhabu

  Traore alichezea klabu hiyo ya Mali katika msimu wa 2015 na CAF ikafungia mechi nne, lakini akatumia adhabu ya mechi moja na nyingine tatu ilikuwa atumie katika mashindano ya msimu huu kwa mujibu wa kanuni namba 114.1 na 114.2 ya Adhabu ya CAF.
  Pamoja na hayo, AS Vita ikamchezesha katika mechi za hatua za awali za Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Mafunzo ya Zanzibar.
  Kwa kutumia kanuni ya VII aya ya 9 na 10 ya kanuni za Ligi ya Mabingwa katika masuala ya kinidhamu, Kamati imeamua kuiondoa mashindanoniAS Vita na nafasi yake itachukuliwa na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, wapinzani wa mwisho kutolewa na timu hiyonya DRC katika hatua za awali.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: AS VITA YAENGULIWA LIGI YA MABINGWA KWA KUTUMIA ALIYEFUNGIWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top