• HABARI MPYA

  Alhamisi, Mei 26, 2016

  YANGA NA AZAM KATIKA PICHA JANA UWANJA WA TAIFA

  Beki wa Yanga, Kevin Yondan (kushoto) akimiliki mpira pembeni ya mshambuliaji wa Azam FC, John Bocco katika mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Kombe la Azam Sports Federation Cup Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Yanga ilishinda 3-1
  Beki wa Yanga, Juma Abdul (kushoto) akimdhibiti winga wa Azam FC, Farid Mussa jana
  Kiungo wa Yanga, Haruna Niyonzima akimtoka beki wa Azam FC jana
  Miguu mitatu ikiwania kuupiga mpira mmoja, wa Bocco (kulia), beki wa Yanga, Vincent Bossou (katikati) na Farid Mussa (kushoto)

  Mshambuliaji wa Yanga, Donald Ngoma akijivuta kupiga mpira baada ya kumuacha kiungo wa Azam FC, Jean Baptiste Mugiraneza  

  Kiungo wa Azam FC, Mudathir Yahya akimtoka kiungo wa Yanga, Thabani Kamusoko

  Kiungo wa Yanga, Deus Kaseke akiupigia hesabu mpira mbele ya kiungo wa Azam FC, Himid Mao

  Beki wa Yanga, Juma Abdul (kushoto) akinyoosha mguu kwa kasi kuuzuia mpira uliopigwa na winga wa Azam FC, Farid Mussa

  Mshambuliaji wa Azam FC, John Bocco akipambana kupenya katikati ya mabeki wa Yanga, Boccou na Yondan (kushoto)

  Rais wa TFF, Jamal Malinzi (kulia) akisalimiana na makocha wa Yanga, JUma Mwambuai na Hans van der Pluijm
  Ofisa wa Azam TV akiwavalisha Medali za ushindi wa Kombe la ASFC wachezaji wa Azam FC
  Rais wa TFF, Jamal Malinzi akimvalisha Medali beki wa Yanga, Kevin Yondan

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: YANGA NA AZAM KATIKA PICHA JANA UWANJA WA TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top