• HABARI MPYA

    Tuesday, May 10, 2016

    HAJIB ABADILISHIWA TIMU SAUZI, SASA APELEKWA AMAZULU

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    MENEJA wa wanamichezo mbalimbali nchini, Juma Ndabila amesema kwamba mshambuliaji wa Simba SC, Ibrahim Hajib ataanza majaribio Jumatatu katika klabu ya AmaZulu ya Ligi Kuu ya Afrika Kusini.
    Tayari Hajib na Ndabile wapo, Durban makao makuu ya klabu hiyo baada ya kuwasili, jana wakitokea Dar es Salaam.
    "Mipango ya awali ilikuwa tumlete Kaizer Chiefs, lakini huyu wakala huku kasema bora aanzie AmaZulu ambako ana nafasi kubwa ya kufanikiwa,"amesema Ndabila.
    Hajib aliondoka nchini jana asubuhi, ikiwa ni siku moja tangu atolewe kwa kadi nyekundu katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara timu yake, Simba ikilala 1-0 mbele ya Mwadui FC ya Shinyanga Uwanja wa Taifa, Jumapili.
    Ibrahim Hajib (kulia) wakati anaondoa jana Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam  
    Na kwa sababu kwa kadi Hajib asingeweza kucheza mechi mbili kati ya tatu za mwisho za Simba, akapna ni wakati mwafaka kutimiza mpango wake wa kwenda kujaribu bahati yake sehemu nyingine. 
    Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amesema kwamba uongozi haufahamu lolote kuhusu safari ya Hajib.
    Aidha, Poppe amesema kwamba lakini hawana waiwasi kwa sababu mchezaji huyo ana Mkataba wa mwaka mmoja zaidi Simba. Kila la heri kwa Hajib
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: HAJIB ABADILISHIWA TIMU SAUZI, SASA APELEKWA AMAZULU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top