• HABARI MPYA

    Wednesday, November 04, 2015

    MICHUANO YA KOMBE LA SHIRIKISHO KUANZA NOVEMBA 8

    RAUNDI YA KWANZA KOMBE LA SHIRIKISHO LA AZAM
    Novemba 8, 2015
    Kariakoo Vs Changanyikeni
    Wenda FC Vs Madini FC
    JKT Rwankoma Vs Villa Squad
    Novemba 10, 2015
    Sabasaba FC Vs Abajalo Tabora
    Milambo Fc Vs The Mighty Elephant
    Novemba 11, 2015
    Mkamba Rangers Vs Mvuvumwa
    Singida United Vs Bulyakhulu SC
    Abajalo Dar Vs Transit Camp
    Novemba 21, 2015
    Pamba SC Vs Polisi Dodoma
    AFC Vs Polisi Mara
    Novemba 22, 2015
    Panone Fc Vs Cocacola Kwanza
    Magereza Iringa Vs Polisi Dar
    Novemba 23, 2015
    Polisi Tabora Vs Green Warriors
    Novemba 24, 2015
    Rhino Rangers Vs Alliance
    Novemba 25, 2015
    Ruvu Shooting Vs Cosmopolitan
    Novemba 26, 2015
    Polisi Moro Vs Mshikamano
    Rhino Rangers wataanza na Alliance Novemba 24, mwaka huu

    MICHUANO ya Kombe la Shirikisho ya Azam Sports inafunguliwa rasmi Jumapili (Novemba 8, 2015) kwa mechi tatu zitakazochezwa kwenye viwanja vitatu tofauti.

    Mechi rasmi ya ufunguzi itakuwa kati ya wenyeji JKT Rwamkoma ya Mara na Villa Squad ya Dar es Salaam itakayofanyika kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume mjini Musoma.
    Siku hiyo pia kutakuwa na mechi kati ya Kariakoo ya Lindi na Changanyikeni FC ya Dar es Salaam itakayochezwa kwenye Uwanja wa Ilulu mjini Lindi, wakati Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Wenda FC ya Mbeya na Madini SC ya Arusha.
    Bingwa wa michuano hiyo inayodhaminiwa na Azam Sports HD ataiwakilisha Tanzania kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika mwaka 2017.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MICHUANO YA KOMBE LA SHIRIKISHO KUANZA NOVEMBA 8 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top