• HABARI MPYA

    Thursday, November 05, 2015

    ARSENAL YABEBESHWA ‘KIZIGO’ MUNICH, YACHAPWA 5-1, CHELSEA NA BARCA ZANG’ARA

    MATOKEO LIGI YA MABINGWA ULAYA
    Novemba 4, 2015  
    Bayern Munich 5-1 Arsenal
    Chelsea 2-1 Dynamo Kyiv
    Barcelona 3-0 BATE Borisov
    Olympiakos 2-1 Dinamo Zagreb
    Roma 3-2 Bayer 04 Leverkusen
    Novemba 3, 2015
    Shakhtar Donetsk 4-0 Malmo FF
    B. Monchengladbach 1-1 Juventus
    Benfica 2-1 Galatasaray
    Real Madrid 1-0 Paris Saint-Germain
    Sevilla 1-3 Manchester City
    PSV 2-0 VfL Wolfsburg
    Manchester United 1-0 CSKA Moscow
    FC Astana 0-0 Atletico de Madrid
    Robert Lewandowski akiifungia bao la kwanza kiulaini Bayern Munich dhidi ya Bayern Munich  PICHA ZAIDI GONGA HAPA

    ARSENAL imebebeshwa ‘mzigo wa maana’ baada ya kuchapwa mabao 5-1 na Bayern Munich katika mchezo wa Kundi F Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku huu Uwanja wa Allianz Arena.
    Mabao na Bayern yamefungwa na Robert Lewandowski dakika ya 10, Thomas Muller dakika ya 29 na 89, David Alaba dakika ya 44 na Arjen Robben dakika ya 55, wakati bao pekee la Arsenal limefungwa na Olivier Giroud dakika ya 69.
    Mchezo mwingine wa kundi hilo, Olympiakos imeshinda 2-1 dhidi ya Dinamo Zagreb, mabao yake yakifungwa na Felipe Pardo yote dakika ya 65 na 90, bao la wageni likifungwa na Armin Hodzic dakika ya 21 Uwanja wa Georgios Karaiskakis.
    Chelsea imeshinda 2-1 dhidi ya Dynamo Kyiv katika mchezo wa Kundi G Uwanja wa Stamford Bridge.
    Luis Suarez akishangilia baada ya kuifungia Barcelona bao la pili dhidi ya Bate Borisov Uwanja wa Nou Camp  PICHA ZAIDI GONGA HAPA

    Chelsea ilinufaika na bao la kujifunga la Aleksandar Dragovic dakika ya 34 kabla ya Willian Borges Da Silva kufunga la pili dakika ya 83, wakati bao pekee la Dynamo limefungwa na Aleksandar Dragovic dakika ya 77. Mchezo mwingine wa Kundi hilo, Porto imeshinda ugenini 3-1 dhidi ya Maccabi Tel Aviv.
    Barcelona imeshinda 3-0 dhidi ya BATE Borisov katika mchezo wa Kundi E Uwanja wa Camp Nou, mabao ya Neymar da Silva Santos Junior kwa penalti dakika ya 30, Luis Suarez dakika ya 60 na Neymar da Silva Santos Junior dakika ya 83.
    Mchezo mwingine wa kundi hilo, Roma imeshinda  3-2 dhidi ya Bayer 04 Leverkusen. Mabao ya Roma yamefungwa na Mohamed Salah dakika ya pili, Edin Dzeko dakika ya 29 na Miralem Pjanic kwa penalti dakika ya 80, wakati ya Bayer yamefungwa na Admir Mehmedi dakika ya 46 na Javier Hernandez ‘Chicharuito’ dakika ya 51. 
    Willian akiifungia Chelsea bao la ushindi dhidi ya Dynamo Kiev Uwanja wa Stamford Bridge PICHA ZAIDI GONGA HAPA
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ARSENAL YABEBESHWA ‘KIZIGO’ MUNICH, YACHAPWA 5-1, CHELSEA NA BARCA ZANG’ARA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top