• HABARI MPYA

    Monday, October 06, 2014

    MTAALAMU WA FIFA AJA KUWAFUNDA MAKOCHA 32 KOZI YA OLIMPIKI

    Na Boniface Wambura, DAR ES SALAAM
    MAKOCHA 32 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar watahudhuria kocha ya ukocha ya ngazi pevu (advance) iliyoandaliwa na Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) kupitia Olympic Solidarity kwa ushirikiano na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) itakayofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba 13 mwaka huu.
    Kozi hiyo itakayomalizika Oktoba 25 mwaka huu itaendeshwa na Mkufunzi wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) Ulrich Marriot kutoka Shelisheli, na makocha wanatakiwa kuripoti hosteli za TFF zilizopo Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Oktoba 12 mwaka huu jioni.
    Kocha wa Stand United, Athumani Bilal wa pili kulia

    Makocha hao ni Ahmed Suleiman Simba (Alliance), Akida Saidi (Lindi), Ally Bushir Mahmoud (Zanzibar), Aloyce Akwilin (Pwani), Amin Rashid Mdowe (Zanzibar), Augustino Dakto Damian (Katavi), Athuman Bilal (Shinyanga), Bakari Shime (Tanga), Charles Mayaya (Shinyanga) na Choki Abeid (Geita).
    Edna Lema (Morogoro), George Melchior (Kagera), Godfrey Kapufi (Katavi), Hamis Mabo (Kigoma), Hawa Bajangero (TWFA), Ibrahim Mulumba (Geita), Jemedari Said (TAFCA), Kenny Mwaisabula (TAFCA), Madenge S. Omari (Mara), Milambo Camil (Tabora) na Mohamed D (Ruvuma).
    Mohamed Ismail Laiser (Manyara), Mohamed Muya (Dodoma), Ngawina Ngawina (Mtwara), Nicholas Kiondo (Ilala), Osuri Charles Kosuri (Simiyu), Rachel Palangyo (TWFA), Salvatory Edward (Temeke), Seif Bausi Nassor (Zanzibar), Yusuf Macho (Kigoma), Wilfred Mollel (Iringa) na Zacharia Mgambwa (Rukwa).
    Makocha watakaofaulu kozi hiyo watapewa Leseni C za ukocha za Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).  
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MTAALAMU WA FIFA AJA KUWAFUNDA MAKOCHA 32 KOZI YA OLIMPIKI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top