• HABARI MPYA

    Monday, October 06, 2014

    MAXIMO ASEMA SIMBA SC HAWAMNYIMI USINGIZI…AWAAHIDI ZAWADI YA KICHAPO OKTOBA 18 TAIFA

    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    KOCHA Mkuu wa Yanga SC, Mbrazil Marcio Maximo amesema kwamba hawahofii Simba SC na ana imani na kikosi chake kitaibuka na ushindi dhidi yao katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Oktoba 18, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

    Kocha wa Yanga SC, Mbrazil Marcio Maximo amesema kwamba hawahofii Simba SC na ana matumaini ya kuwafunga Oktoba 18, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa Ligi Kuu

    REKODI YA MAXIMO YANGA SC 

    Yanga SC 1-0 Chipukizi (kirafiki Pemba)
    Yanga 2-0 Shangani (kirafiki Zanzibar)
    Yanga SC 2-0 KMKM (Kirafiki Zanzibar)
    Yanga SC 1-0 Thika United (Kirafiki Taifa)
    Yanga SC 3-0 Azam FC (Ngao ya Jamii)
    Yanga SC 0-2 Mtibwa Sugar (Ligi Kuu)
    Yanga SC 2-1 Prisons (Ligi Kuu)
    Yanga SC 2-1 JKT Ruvu (Ligi Kuu)
    Akizunguma na BIN ZUBEIRY jana mjini Dar es Salaam, Maximo alisema hawahofii kabisa Simba SC bali anawapa heshima yao kama timu nzuri yenye kocha mzuri, Mzambia, Patrick Phiri.
    “Naifahamu Simba ni timu nzuri, timu kubwa, namfahamu kocha Phiri. Ni kocha mzuri na mzoefu. Lakini siwahofii kabisa na wala huwa siogopi mechi ya upinzani. Kumbuka niliwafunga Azam,”amesema.
    Maximo anatarajia mchezo huo utakuwa mgumu kwa sababu utakutanisha timu zenye mashabiki wengi nchini, lakini amewataka wana Yanga wawe na imani na timu yao.
    Alipoulizwa kuhusu kiu ya Yanga SC kulipa kisasi cha 5-0 walizopigwa mwaka 2011, Maximo amesema; “Mimi nachotaka ni ushindi tu, siyo kushinda mabao mangapi. Muhimu ushindi na pointi tatu,”amesema.
    Yanga SC imeshinda mechi mbili mfululizo, lakini mara zote nyavu zao zimetikiswa (2-1 na Prisons na JKT Ruvu), kuhusu hilo Maximo anasema; “Wakati wote baada ya mechi tunakwenda kufanyia kazi mapungufu yetu, tunaendelea kufanyia kazi hilo, tunataka kushinda bila kufungwa,”.
    Yanga SC itakutana na Simba SC ambayo haijashinda mechi hata moja msimu huu baada ya kutoa sare mechi zake zote tatu, 2-2 na Coastal Union ya Tanga, 1-1 na Polisi Moro na 1-1 na Stand United ya Shinyanga iliyopanda Ligi Kuu msimu huu.
    Yanga SC yenyewe imeshinda mechi mbili 2-1 na Prisons ya Mbeya na 2-1 na JKT Ruvu ya Pwani, baada ya kupoteza mchezo wa kwanza kwa kufungwa 2-0 na Mtibwa Sugar mjini Morogoro. 
    Hadi sasa, Maximo amekwishaiongoza Yanga SC katika mechi nane tangu aanze kazi Julai mwaka huu akirithi mikoba ya Mholanzi, Hans van der Pluijim na kati ya hizo amepoteza moja tu dhidi ya Mtibwa.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAXIMO ASEMA SIMBA SC HAWAMNYIMI USINGIZI…AWAAHIDI ZAWADI YA KICHAPO OKTOBA 18 TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top