KIASI cha wiki mbili zilizopita, bendi ya Malaika ilimpoteza mwimbaji wake mpya Adaya Nzinga aliyefariki kwa ugonjwa wa malaria.
Ijumaa iliyopita mwanamuziki mkongwe na bingwa wa kupuliza saxophone, Ally Rashid wa Msondo Ngoma naye akaaga dunia baada ya kuugua ugonjwa wa kupooza kwa miaka kadhaa.
Adaya Nzinga alizikwa makaburi ya Kinondoni na Ally Rashid akazikwa makaburi ya Keko Machungwa. Nimezidi kujifunza somo la ajabu kufuatia vifo vya wasanii hawa.
Tuanze na Adaya Nzinga wa Malaika Band. Kuna bendi inaitwa Victoria Sound ambayo ni ndugu moja na Malaika Band kwa maana ya kumilikiwa na mtu mmoja – kwa lugha nyingine unaweza kusema wasanii wa Malaika na Victoria Sound wako katika ofisi moja.
Wakati tukimhifadhi Adaya Nzinga pale makaburi ya Kinondoni, sikubahatika kumuona msanii hata mmoja wa Victoria Sound na si hapo tu bali hata kwenye msiba pale Vijana Social Hall bado hakuonekana msanii wa Victoria Sound.
Inapotekea wafanyakazi wa ofisi moja hawazikani huwa inaacha maswali mengi sana, binafsi bado sijaelewa wasanii wa Victoria Sound wamelenga kutufunza kitu gani juu ya msiba wa Adaya Nzinga.
Tena mbaya zaidi ni kwamba Victoria Sound walikacha mazishi ya msanii wa Malaika Band ambao walikuwa wasindikizaji wa onyesho lao la utambulisho wa ujio wao mpya pale New Msasani Club siku chache baada ya kifo cha Adaya Nzinga.
Bado haieleweki sababu ya wasanii wa dansi na taarab kuwa nyuma katika kuzikana – pengine ni roho mbaya, labda ukosefu wa nauli, au huenda ni uvivu, inaweza pia ni kutoamini kuwa siku moja nao watakufa na kuhitaji kuzikwa.
Turejee kwa Ally Rashid wa Msondo Ngoma. Huyu hadi anaanza kuugua alikuwa ni mwanamuziki wa Msondo na hata ukifuatilia historia ya kuugua kwake utagundua kuwa alianza kuugua akiwa kazini kwenye maonyesho ya Msondo. Hakupita bendi nyingine tena hadi anafariki.
Unajua watu wangapi wa Msondo waliofika makaburini kumzika mfanyakazi mwenzao Ally Rashid? Ni wawili tu – Said Kibiriti na Zahoro Bangwe.
Ally Rashid alifariki Ijumaa mchana na jioni yake Msondo wakawa na onyesho la kufungua shamra shamra za miaka 50 ya bendi yao pale Leaders Club, onyesho liliendelea kama kawaida, siwalaumu kwa kutokatisha onyesho hilo maana pengine kifo cha mfanyakazi wao kimekuja muda mfupi kabla ya onyesho ambalo bila shaka liligharimu senti nyingi kuliandaa.
Lakini nilitegemea wangetumia onyesho hilo kuhamasishana kwenda kumzika mwenzao kesho yake. Kihalali Msondo Ngoma walistahili kuhusika kwenye mazishi ya Ally Rashid kwa hali na mali, lakini mimi leo nazungumzia kwa HALI tu, sitaki kabisa kuzungumzia mambo ya MALI, sielewi kwanini walishindwa kwenda kumzika msanii mwenzao, nazidi kuamini kuwa kwa mwendo huu hakuna mtoto atakayetamani kuwa mwanamuziki wa dansi.
Labda niwaguse kidogo na wasanii wa taarab. Ally Rashid alikuwa baba mzazi wa mwimbaji wa taarab Mwanahawa Ally Chipolopolo, nilitegemea kuona wasanii wengi wa taarab makaburini wakimzika baba wa msanii mwenzao wa taarab, lakini haikuwa hivyo.
Hebu jifunzeni kupitia msiba wa baba mzazi wa msanii wa bongo movie Single Mtambalike “Rich Rich” , aliyezikwa Jumamosi na kuhudhuriwa na wasanii wengi sana wa tasnia ya filamu. Oneni aibu kidogo.
Baada ya mazishi ya Ally Rashid, mzee King Kiki aliwakusanya wanamuziki wa dansi waliohudhuria mazishi hayo na kuwaomba wapendane na kuwa na umoja. Mimi binafsi niliguna, niliguna kwa kuwa huo umekuwa wimbo wa kila siku. Hakuna kuzikana, hakuna kuuguzana - umoja utatoka wapi? Tukutane Jumatatu ijayo.

0 comments:
Post a Comment