Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
YANGA SC imeingia kambini leo katika hoteli ya Landmark, Kunduchi, Dar es Salaam kujiandaa na mchezo dhidi ya mahasimu wao wa jadi, Simba SC Jumamosi ijayo Uwanja wa Taifa, Jijini.
Kocha Mkuu wa Yanga SC, Mbrazil Marcio Maximo ameingia kambini na wachezaji 28 na timu itakuwa ikifanya mazoezi Uwanja wa Boko Veterani, ambao ulikuwa unatumiwa na mahasimu wao hao awali.
Maximo, kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars amesema vijana wake wote wapo katika hali nzuri kiafya, kifikra na morali ipo juu kuelekea kwenye mechi hiyo.
“Natambua mechi za wapinzani wa jadi huwa hazitabiriki, ila sisi kama Yanga tunajiandaa kuhakikisha tunapata ushindi katika mchezo huo dhidi ya Simba SC siku ya jumamosi, makosa yaliyokuwa yakijitokeza katika michezo iliyopita tumeshayafanyia kazi” Maximo amekaririwa na tovuti ya Yanga akisema.
Wachezaji waliongia kambini Yanga SC ni makipa; na Deo Munishi ‘Dida’, Juma Kaseja na Ally Mustafa ‘Barthez’, mabeki Juma Abdul, Salum Telela, Oscar Joshua, Amos Abel, Edward Charles, Rajab Zahir, Pato Ngonyani, Kevin Yondan na Nadir Haroub ‘Cannavaro’, viungo Mbuyu Twite, Said Juma ‘Kizota’, Omega Seme, Hamisi Thabit, Nizar Khalfan, Issa Ngao na Haruna Niyonzima wakati washambuliaji ni Genilson Santana Santos ‘Jaja’, Andrey Coutinho, Said Bahanuzi, Hamisi Kiiza, Simon Msuva, Mrisho Ngassa, Hussein Javu na Jerry Tegete.
Wakati Yanga SC wakiingia kambini Dar es Salaam, wapinzani wao, Simba SC wako Afrika Kusini tangu wiki iliyopita kwa maandalizi ya mchezo huo, unaotarajiwa kuwa mkali na wa kusisimua.

![]() |
Kikosi cha Yanga SC kimeingia kambini leo kujiandaa na mechi na Simba SC Jumamosi |

0 comments:
Post a Comment