Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
FAINALI ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka huu itazikutanisha ES Setif ya Algeria na AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), mchezo wa kwanza ukifanyika Uwanja wa Mei 8 1945 mjini Setif Oktoba 24 na marudiano Uwanja wa Martyrs, Kinshasa Oktoba 31.
Vita iliitoa CS Sfaxien kwa jumla ya mabao 4-2 ikishinda 2-1 nyumbani na ugenini, wakati Setif iliwatoa TP Mazembe ya DRC pia kwa mabao ye ugenini, baada ya sare ya jumla ya 4-4, ikishinda 2-1 nyumbani na kufungwa 3-2 ugenini.
IJUE AS VITA ILIYOFUFUA MAKALI:
Association Sportive Vita Club, inayojulikana tu kama AS Vita Club, AS V. Club au kwa urahisi zaidi Vita Club, ni miongoni mwa klabu kongwe DRC yenye maskani yake mjini Kinshasa.
AS Vita ilianzishwa mwaka 1935 na Honore Essabe ikitumia jina la Renaissance Usoke mjini Kinshasa.
Jina hilo lilibadilika mwaka 1939 na kuwa Diables Rouges, kabla ya mwaka 1942 kuanza kutumia jina la Victoria Club na hatimaye mwaka 1971 wakaanza kutumia jina Vita Club, ambalo wanaendelea nalo hadi leo.
AS Vita imeshinda mataji kibao DRC, yakiwemo sita ya Ligi ya jimbo la Kinshasa katika miaka ya 1957, 2001, 2002, 2004, 2005 na 2009, Super Cup ya Kinshasa mara tatu 2002, 2005 na 2006 ubingwa wa Ligi Kuu ya DRC mara 12 katika miaka ya 1970, 1971, 1972, 1973, 1975, 1977, 1980, 1988, 1993, 1997, 2003 na 2010 na Kombe la Kongo mara tisa katika miaka ya 1971, 1972, 1973, 1975, 1977, 1981, 1982, 1983 na 2001.
Katika michuano ya Afrika, AS Vita ndiyo mabingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 1973 wakati mwaka 1981 walishika nafasi ya pili.
Vita wamecheza mara nane Klabu Bingwa Afrika kati ya mwaka 1971 na 1995 na ilipobadilishwa jina kuwa Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 1997, wamecheza mara sita tangu 1998 hadi sasa.
Zaidi ya ubingwa, mafanikio mengine makubwa awali ya Vita katika Ligi ya Mabingwa ni kufika Nusu Fainali mwaka 1978, Fainali 1981 na mafanikio yao ya mwaka huu ni matunda ya uvumilivu tangu hapo, kwani mwaka jana walitolewa raundi ya kwanza tu.
Katika Kombe la Shirikisho, Vita wamecheza mara tatu tu 2008 wakitolewa Raundi ya Kwanza, 2009 waliingia kwenye makundi kabla ya 2010 kutolewa Raundi ya Kwanza. Wakati michuano hiyo bado inaitwa Kombe la CAF, walishiriki mara mbili, mwaka 1996 wakifika Nusu Fainali na 1999 wakiishia raundi ya pili.
Iliyokuwa michuano ya Kombe la Washindi walicheza mara sita mwaka 1976 wakifika Nusu Fainali, 1979, 1982, 1983 na 2002 mara zote hizo wakienda Robo Fainali.
Kwa sasa, Vita inayojulikana pia kwa jina la utani, Les Dauphins Noirs yaani Pomboo Mweusi (samaki aina ya nyangumi) iko chini ya Rais, Gabriel Amisi Kumba na kocha Florent Ibenge.
Kikosi cha sasa; Itoua Old, Mabele Bawaka, Simbi Patou Ebunga, Nkanu Walby Niemba, Chikito Lema Mabidi, Munganga Nelson, Basilua Jeremie, Ilonga Ilifo, Djiibeogo Abdoul Aziz, Ndaya Mbangi, Heritier Luvumbu Nzinga, Mpanda Yves Magola, Mutambala Lomalisa, Mampuya Patrick Lema, Nelson Lukong (Cameroon), Kasereka Thierry, Ndombe Mbala, Firmin Ndombe Mubele, Dido Bafola(Kongo Kinshasa), Emmanuel Ngudikama, Kasengu Kazadi, Tady Etekiama, Tchimanga Dady Mutamba, Mvete Luyeye, Ngoyi Emomo Eddy, Lomboto Nguemba, Kisombe Mundaba, Mayele Vivien, Makiadi Pambani, Kupa Makwekwe, Geyi Ndemiye, Guy Lusadisu Basisila, Paolo Mondo (Cameroon), Hamidou Abdoul Rahim (Cameroon), Mputu Mbungu Serge, Landu Nkuwu, Botayi Bamoto, Déo Kanda na Ibara Franchel (Kongo Kinshasa).

0 comments:
Post a Comment