HISPANIA imeichapa mabao 4-0 Luxembourg katika mchezo wa Kundi C kufuzu Euro 2016 usiku jana ugenini.
Katika mchezo huo, ambao kipa Iker Cassilas wa Real Madrid alipumzishwa akimpisha David de Gea wa Manchester United, kiungo wa Manchester City, David Silva alifunga bao la kwanza dakika ya 27 kabla ya Paco Alcacer kufunga la pili dakika ya 42.
Diego Costa, aliyepoteza nafasi za kufunga kipindi cha kwanza, hatimaye akafungua akaunti yake mabao timu ya taifa kwa bao la dakika ya 69, kabla ya Juan Bernat aliyetokea benchi kufunga la nne dakika ya 88.
Costa anafunga bao lake la kwanza kwa nchi yake hiyo ya kuhamia baada ya dakika 515 za kuichezea bila kuifungia. Katika mechi nyingine za Kundi C, Ukrine iliichapa FYR Macedonia 1-0 bao pekee la Sydorchuk dakika ya 45 wakati Slovakia iliichapa 3-1 Belarus.
Kundi G, Austria imeifunga 1-0 Montenegro, Urusi imetoka 1-1 Moldova na Sweden imeifunga 2-0 Liechtenstein.
Kikosi cha Luxembourg kilikuwa: Joubert, Mutsch, Chanot, Martins Pereira/Turpel dk60, Philipps, Janisch, Jans, Gerson, Holter, Da Mota Alves/Payal, dk75 na Bensi.
Hispania: De Gea, Pique, Bartra, Jordi Alba, Carvajal, Busquets, Iniesta/Bernat dk72, Koke, Silva/Pedro, dk71, Alcacer na Costa/Rodrigo, dk83.

![]() |
Diego Costa akipongezwa na wenzake baada ya kufunga jana |
0 comments:
Post a Comment