• HABARI MPYA

    Sunday, October 05, 2014

    FALCAO AFUNGUA AKAUNTI YA MABAO MAN UNITED IKIICHAPA EVERTON 2-1, DE GEA AOKOA PENALTI

    MANCHESTER United imepata ushindi wa pili mfululizo katika Ligi Kuu ya England, baada ya kuichapa mabao 2-1 Everton Uwanja wa Old Trafford jioni hii.
    Hali sasa ni shwari kwa kocha Louis Van Gaal baada ya ushindi huo- mshambuliaji wake wa mkopo, Radamel Falcao akifunga bao lake la kwanza tangu atue Old Trafford. 
    Angel di Maria alitangulia kuifungia Manchester United dakika ya 26 kabla ya mkwaju wa penalti wa Leighton Baines kuokolewa na David de Gea dakika ya 45 baada ya Tony Hibbert kuchezewa rafu na Luke Shaw. 
    Everton ilisawazisha bao hilo dakika ya 55 kupitia kwa Steven Naismith akimalizia krosi nzuri ya Baines kabla ya Radamel Falcao kuifungia bao la ushindi Manchester United dakika ya 62.
    Radamel Falcao akishangilia baada ya kuifungia Man United bao la ushindi
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: FALCAO AFUNGUA AKAUNTI YA MABAO MAN UNITED IKIICHAPA EVERTON 2-1, DE GEA AOKOA PENALTI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top