• HABARI MPYA

    Sunday, October 05, 2014

    PARK JI-SUNG ALA SHAVU MAN UNITED, AINGIA KWENYE ORODHA YA WATU SITA MUHIMU OLD TRAFFORD

    KIUNGO wa zamani wa Manchester United, Park Ji-sung ametambulishwa kuwa Balozi wa klabu Old Trafford leo akiungana na aliyekuwa kocha wake, Sir Alex Ferguson.
    Wawili hao walifanyiwa mahojiano uwanjani kabla ya United kuanza kupepetana na Everton, na Ferguson akazungumzia enzi za Park na umuhimu aliokuwa nao Manchester. 
    Uteuzi huo wa Park unafanya idadi ya Mabalozi wa United kufika sita, baada ya Sir Bobby Charlton, Andrew Cole, Ferguson, Denis Law na Bryan Robson.

    Park Ji-sung (kushoto) akiwa na Sir Alex Ferguson wakati wa utambulisho wake wa kuwa Balozi wa klabu hiyo leo
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: PARK JI-SUNG ALA SHAVU MAN UNITED, AINGIA KWENYE ORODHA YA WATU SITA MUHIMU OLD TRAFFORD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top