• HABARI MPYA

    Thursday, October 09, 2014

    DIEGO COSTA FITI KABISA KUITUMIKIA HISPANIA MECHI ZA KUFUZU EURO 2016

    MSHAMBULIAJI Diego Costa hajaonyesha dalili zozote za kusumbuliwa na tatizo lake sugu la maumivu ya nyama akifanya mazoezi na timu yake ya taifa, Hispania kuelekea mechi za kufuzu Euro 2016 dhidi ya Slovakia na Luxembourg.
    Mpachika mabao huyo wa Chelsea alikuwa pamoja na wachezaji wen sake wa Cesc Fabregas anayecheza naye The Blues, na wengine wanaochea Ligi Kuu ya England, David Silva na David de Gea. 
    Kikosi cha Vicente del Bosque kiliifumua Macedonia mabao 5-1 katika mchezo wao wa ufunguzi wa kufuzu na sasa kinaelekeza nguvu zake kwa Slovakia na Luxembourg.

    Diego Costa ameonyesha yuko fiti kabisa kuitumikia Hispania katika mechi za kufuzu Euro 2016
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: DIEGO COSTA FITI KABISA KUITUMIKIA HISPANIA MECHI ZA KUFUZU EURO 2016 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top