• HABARI MPYA

    Friday, October 03, 2014

    DEMBA BA AIPOKONYA TONGE MDOMONI SPURS WHITE HART LANE

    MSHAMBULIAJI wa zamani wa Chelsea, Demba Ba usiku huu amefunga kwa penalti kuipatia timu yake Beskitas sare ya 1-1 ugenini na Tottenham Hotspur Uwanja wa White Hart Lane katika mchezo wa Kundi C Europa League.
    Demba alifunga penalti hiyo dakika ya 89, akimtungua kipa hodari Hugo Lloris baada ya Vlad Chiriches kuunawa mpira kwenye boksi.
    Tottenham ilipata bao lake mapema dakika ya 27 kupitia kwa Harry Kane na Lloris alijitahidi kuulinda ushindi huo kwa kuokoa michomo mingi ya hatari, kabla ya Chiriches kuwazawadia penalti wapinzani. 

    Demba Ba akishangilia baada ya kuisawazishia Besiktas katika Europa League dhidi ya Tottenham Uwanja wa White Hart Lane
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: DEMBA BA AIPOKONYA TONGE MDOMONI SPURS WHITE HART LANE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top