• HABARI MPYA

    Friday, October 03, 2014

    MAN UNITED WAMALIZANA NA FALCAO MKATABA BINAFSI WA KUBAKI MOJA KWA MOJA OLD TRAFFORD

    KLABU ya Manchester United tayari imekubali vipengele vya Mkataba binafsi kumsajili moja kwa moja mshambuliaji wake wa mkopo, Radamel Falcao kukwepa kurudia makos a iliyoyafanya kwa Carlos Tevez miaka mitano iliyopita.
    United imemsajili mshambuliaji huyo wa kati wa Colombia kwa mkopo kutoka Monaco katika siku ya mwisho ya kufunga pazia la usajili.
    Ikiwa imetoa Pauni Milioni 6 kwa klabu ya Ufaransa kwa ajili ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28, United pia imekubali kulipa ada ya uhamisho wa jumla ya Pauni Milioni 43.5 iwapo wataamua kumchukua moja kwa Falcao mwishoni mwa msimu.
    Inafahamika Manchester United imekubali kumlipa mshahara wa Pauni 250,000 kwa wiki mchezaji huyo.

    Manchester United imekubaliana vipengele binafsi vya mkataba na Radamel Falcao kwa ajili ya kumsajili moja kwa moja
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAN UNITED WAMALIZANA NA FALCAO MKATABA BINAFSI WA KUBAKI MOJA KWA MOJA OLD TRAFFORD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top