Na Boniface Wambura, DAR ES SALAAM
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limefahamishwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kuwa Tanzania haitaweza kuwa mwenyeji wa Fainali za Afrika- AFCON 2017 kwa kuwa haijawahi kuandaa fainali zozote za vijana Afrika. Fainali hizo ni zile za vijana wenye umri chini ya miaka 17 na 20.
Hivyo, TFF inaelekeza nguvu zote katika kuandaa Fainali za Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka U17 mwaka 2019.
“Tunapenda kuchukua fursa hii kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanazania, Jakaya Kikwete kwa kututia moyo katika kuomba uenyeji wa AFCON 2017,”imesema taarifa ya TFF.
“Pia tunamshukuru Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk Fenella Mukangara kwa juhudi binafsi alizozionyesha katika jitihada za Tanzania kuomba uenyeji wa AFCON 2017,” imeongeza taarifa hiyo.
TFF imesema inaamini kwa dhati kuwa uenyeji wa Afrika U17 2019 utaifungulia Tanzania milango ya kuandaa mashindano makubwa zaidi.

![]() |
| Mshambuliaji wa Tanzania, Mbwana Samatta akipasua katikati ya mabeki wa Msumbiji katika mechi ya kufuzu AFCON mwakani Morocco. Tanzania ilitolewa. |
“Pia tunamshukuru Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk Fenella Mukangara kwa juhudi binafsi alizozionyesha katika jitihada za Tanzania kuomba uenyeji wa AFCON 2017,” imeongeza taarifa hiyo.
TFF imesema inaamini kwa dhati kuwa uenyeji wa Afrika U17 2019 utaifungulia Tanzania milango ya kuandaa mashindano makubwa zaidi.

.png)
0 comments:
Post a Comment