• HABARI MPYA

    Tuesday, October 07, 2014

    BEKI LA SIMBA SC LAONGEZWA TAIFA SATRS

    Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
    BEKI wa Simba SC, Joram Mgeveke ameongezwa kwenye kikosi cha timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kitakachomenyana na Benin mwishoni mwa wiki.
    Kwa ujumla, kocha Mholanzi, Mart Nooij ameita wachezaji watatu wapya kutoka 27 alioita awali- ambao ni beki wa kushoto Gardiel Michael wa Azam FC na kiungo Jonas Mkude wa Simba.
    Joram Mgeveke ameongezwa Taifa Stars

    Kikosi kamili Stars sasa kinakuwa; Makipa Deogratias Munishi (Yanga), Aishi Manula (Azam), na Mwadini Ali (Azam).
    Mabeki ni Joram Mgeveke (Simba SC), Gardiel Michael (Azam FC), Said Mourad (Azam), Shomari Kapombe (Azam), Oscar Joshua (Yanga), Nadir Haroub (Yanga), Kelvin Yondani (Yanga), Aggrey Morris (Azam), Miraji Adam (Simba), Charles Edward (Yanga) na Emmanuel Simwanda (African Lyon).
    Viungo ni Jonas Mkude (Simba), Erasto Nyoni (Azam), Mwinyi Kazimoto (Al Markhiya, Qatar), Amri Kiemba (Simba), Himid Mao (Azam), Salum Abubakar (Azam), Said Ndemla (Simba) na Haruna Chanongo (Simba).
    Washambuliaji ni Khamis Mcha (Azam), Simon Msuva (Yanga), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DR Congo), Mbwana Samata (TP Mazembe, DR Congo), Mrisho Ngasa (Yanga), Mwegane Yeya (Mbeya City), na Juma Liuzio (Zesco, Zambia).
    Mechi hiyo ya Kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) itachezeshwa na marefa wa Rwanda Jumapili (Oktoba 12 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Hakizimana Louis ndiye atakayeongoza waamuzi hao wa FIFA kwa kupuliza filimbi, akisaidiwa na Simba Honore na Niyitegeka Jean Bosco.
    Mechi hiyo itatanguliwa na ile ya viongozi wa dini- Kiislamu vs Kikristo kudumumisha upendo, amani na ushirikiano itakayoanza saa 9 kamili alasiri. Tiketi za elektroniki zitakazotumika kwa mechi hiyo tayari zimeanza kuuzwa kwa kiingilio cha sh. 4,000 na sh. 10,000.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BEKI LA SIMBA SC LAONGEZWA TAIFA SATRS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top