• HABARI MPYA

    Thursday, July 03, 2014

    ABDULFATAH ATABIRI LIGI YA MSIMU UJAO ITAKUWA MOTO WA KUOTEA MBALI NA UBINGWA UTAPATIKANA KWA JASHO HASWA

    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    MENEJA wa kipa Juma Kaseja na mdau maarufu wa soka nchini, Abdulfatah Salim Saleh amesema kwamba Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara itakuwa ngumu mno msimu ujao na bingwa atapatikana kwa mbinde.
    Akitoa maoni yake kuelekea msimu ujao wa ligi hiyo, Abdulfatah amesema kwamba kujipanga upya kwa Simba SC, kujiimarisha kwa Yanga SC na kujidhatiti kwa Mbeya City pamoja na ubora wa mabingwa, Azam vinamaansha ligi itakuwa ngumu.
    Abdufatah ametabiri ligi ngumu msimu ujao


    “Azam FC pamoja na kuwa mabingwa, lakini bado wanasajili wachezaji wapya wazuri kuimarisha timu yao, maana yake ubora wao utaongezeka,”.
    “Yanga SC walikuwa wa pili na watu tuliona mwenendo wa ligi, wangeweza kuwa mabingwa, walizidiwa kidogo tu na Azam. Lakini nao wanajiimarisha, wameleta makocha wapya, wanasajili wachezaji wapya. Maana yake wanajiimarisha,”.
    “Simba SC wao wamefanya uchaguzi wamepata viongozi wapya wazuri na wenye uzoefu wa soka ya nchi hii, tarajia kabisa watajenga timu nzuri ya kushindania ubingwa,” amesema Abdulfatah.
    Ameongeza kwamba Mbeya City nao baada ya kupanda msimu uliopita kwa kishindo na kumaliza katika nafasi ya tatu wameanza kuimarisha tena timu yao ili iongeze makali msimu ujao.
    “Sasa hapa tumezungumzia timu nne ambazo moja kwa moja zitaingia kwenye mbio za ubingwa msimu ujao, lakini na timu nyingine nazo pia bila shaka zitajiimarisha. Maana yake ligi ya msimu ujao, kutakuwa na ushindani mkubwa,”amesema.
    Abdulfatah ni mmiliki wa hoteli maarufu ya kisasa, iitwayo Sapphire Court iliyopo Kariakoo mjini Dar es Salaam, ambayo ni maarufu pia kuwa kupokea timu mbalimbali zinazokuja kwenye mashindano ya kimataifa nchini.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ABDULFATAH ATABIRI LIGI YA MSIMU UJAO ITAKUWA MOTO WA KUOTEA MBALI NA UBINGWA UTAPATIKANA KWA JASHO HASWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top