• HABARI MPYA

    Saturday, January 06, 2018

    LIVERPOOL YAKUBALI KUMUUZA COUTINHO PAUNI MILIONI 145

    Philippe Coutinho akiwa mjini London tayari kupanda ndege kwenda Barcelona kukamilisha uhamisho wake wa Pauni Milioni 145 kutoka Liverpool PICHA ZAIDI GONGA HAPA  


    Takwimu za Coutinho Liverpool 

    2012-13 Mechi 13, mabao 3
    2013-14 Mechi 37, mabao 5
    2014-15 Mechi 52, mabao 8
    2015-16 Mechi 43, mabao 12
    2016-17 Mechi 36, mabao 14
    2017-18 Mechi 18, mabao 12 
    KLABU za Liverpool na Barcelona zimekubaliana kuuziana Philippe Coutinho kwa dau la Pauni 145.  
    Picha zimemuonyesha kiungo huyo Mbrazil akisafiri kwenda Hispania kupitia London leo jioni kukamilisha uhamisho. 
    Coutinho, mwenye umri wa miaka 26 anatarajiwa kuishuhiudia Barcelona katika mchezo wa nyumbani wa La Liga na Levante kesho mchana. 
    Akifanikiwa kukamilisha uhamisho huu, atakuwa mchezaji wa pili ghali kihistoria katika ulimwengu wa soka, nyuma ya Mbrazil mwenzake, Neymar, aliyeondoka Barcelona kujiunga na Paris Saint-Germain kwa Pauni Milioni 198 mwanzoni mwa msimu. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: LIVERPOOL YAKUBALI KUMUUZA COUTINHO PAUNI MILIONI 145 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top