• HABARI MPYA

  Wednesday, November 15, 2017

  ITALIA YAMFUKUZA KOCHA BAADA YA KUKOSA KOMBE LA DUNIA

  ITALIA imemfukuza kazi kocha Gian Piero Ventura baada ya kufungwa na Sweden na kutolewa kwenye fainali za Kombe la Dunia.
  Babu huyo wa umri wa miaka ya 69, ameikosesha nchi hiyo maarufu duniani tiketi ya fainali zijazo za Kombe la Dunia kufuatia kutolewa na Sweden, hii ikiwa ni mara ya pili katika historia yao.
  "Hili likiwa ni jambo la kwanza la siku, Rais wa Shirikisho la Soka Italia, Carlo Tavecchio ameamua kwa manufaa ya The Azzurri, kuanzia sasa, Giampiero Ventura si kocha tena wa Ialia. 
  Kocha Gian Piero Ventura amefukuzwa Italia baada ya kufungwa na Sweden na kutolewa kwenye fainali za Kombe la Dunia PICHA ZAIDI GONGA HAPA 

  Tayari FIGC imeingia mafichoni kusaka kocha mbadala na habari zinasema kocha wa zamani wa  Real Madrid na Bayern Munich, Carlo Ancelotti anaweza kuchukua nafasi hiyo.
  Ni mara ya kwanza ndani ya miaka 60 The Azzurri wanakosa fainali za Kombe la Dunia na michuano ya kwanza mikubwa watakosekana tangu walipokosekana kwenye Euro 1992.
  Kufeli kufuzu Kombe la Dunia kumekwenda sambamba na wachezaji wenye umri mkubwa kutangaza kustaafu wakiwemo kipa gwiji, Gianluigi Buffon wakati Daniele De Rossi na Andrea Barzagli wamestaafu pia.
  Ni matumaini kocha mbadala, Ancelotti kwenye umri wa miaka 58 kwa sasa yupo huru baada ya kufukuzwa Bayern Munich mwezi Septemba.

  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ITALIA YAMFUKUZA KOCHA BAADA YA KUKOSA KOMBE LA DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top