• HABARI MPYA

  Thursday, January 14, 2016

  WENGER ATHIBITISHA ARSENAL KUKAMILISHA USAJILI WA MIDO LA MISRI

  KLABU ya Arsenal imekamilisha usajili wa Pauni Milioni 5 wa kiungo wa Misri, Mohamed Elneny kutoka klabu ya Basle ya Uswisi, amethibitisha Arsene Wenger kufuatia sare ya 3-3 jana na Liverpool.
  Mmisri huyo alikamilisha vipimo vya afya wiki iliyopita na sasa anasubiri kupata uhamisho wa kimataifa aungane na wachezaji wenzake wapya wa The Gunners, makao makuu ya timu, Colney, London.
  Wenger sasa amethibitisha kwamba kiungo huyo amekamilisha uhamisho wake kwenda Emirates na anaweza kuwamo katika mchezo ujao Jumapili.

  Arsenal imekamilisha uhamisho wa kiungo wa Misri, Mohamed Elneny kutoka Basle ya Uswisi PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  "Elneny dhahiri amejiunga nasi. Amejiunga nasi,"amesema kocha huyo Mfaransa baada ya sare ya jana Uwanja wa Anfield katika mchezo wa Ligi Kuu ya England.  "Tutaona kama atazufu hadi kufika Jumapili,". 
  Elneny anatarajiwa kuwa mchezaji pekee kusajiliwa na timu hiyo katika dirisha dogo la Januari, ingawa beki wa kulia, Mathieu Debuchy anaweza kuondoka baada ya kumuomba mwenyewe ahame.
  Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 amecheza karibu mechi 100 Basle, akishinda mfululizo mataji ya Ligi Kuu ya Uswisi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WENGER ATHIBITISHA ARSENAL KUKAMILISHA USAJILI WA MIDO LA MISRI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top