• HABARI MPYA

  Saturday, January 02, 2016

  BALOTELLI KUREJEA LIVERPOOL, KLOPP ASHAWISHIWA AMPE NAFASI NYINGINE

  WAKALA Mino Raiola amepanga kufanya mazungumzo na kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp kumshawishi ampe nafasi ya pili mshambuliaji Mario Balotelli Anfield.
  Balotelli yuko kwa mkopo wa muda mrefu AC Milan ambako amecheza mechi nne tu hadi sasa akifunga bao moja kutokana na kufanyiwa upasuaji wa nyonga, ambao umemuweka nje ya Uwanja tangu Septemba.
  Lakini wakala huyo wa kimataifa wa Italia anataka Klopp ampe nafasi ya pili Balotelli Merseyside, licha ya kufunga bao moja tu katika mechi 16 za Ligi Kuu ya England alipokuwa Liverpool msimu uliopita.

  Wakala Mino Raiola (kulia) akiwa na mteja wake, Mario Balotelli ambaye anataka amsukie mipango ya kurejea Liverpool kwa kumshawishi kocha Jurgen Klopp ampe nafasi ya pili Anfield PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  "Kwa kweli. Hiyo ni sehemu ya kazi yangu, kuzungumza na makocha wote,"amesema Raiola akizungumza na Sky. "Namfahamu Klopp tangu (namuwakilisha) Mkhitaryan pale Dortmund.
  "Kama tukizungumzia ubora na kipa, Mario anavyo, hiyo haina swali. Kisha unahitaji kocha ambaye anaamini juu yako na kukupa nafasi ya kuthibitisha mwenyewe. Tutazungumza naye wakati utakapofika,".
  Brendan Rodgers alimsajili Balotelli kutoka AC Milan kwa dau la Pauni Milioni 16 majira ya joto mwaka 2014, baada ya kumpoteza Luis Suarez aliyehamia Barcelona.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BALOTELLI KUREJEA LIVERPOOL, KLOPP ASHAWISHIWA AMPE NAFASI NYINGINE Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top