• HABARI MPYA

  Saturday, July 08, 2023

  NI YANGA NA AZAM, SIMBA NA SINGIDA NGAO YA JAMII TANGA


  SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limetoa Ratiba ya michuano ya Ngao ya Jamii na mabingwa wa mataji yote nchini, Yanga SC watamenyana na Azam FC Agosti 9 huku Simba SC wakimenyana na Singida Fountain Gate Agosti 10 Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.
  Mechi ya Fainali itafuatia Agosti 13 Saa 1:00 usiku ikitanguliwa na mchezo wa kusaka mshindi wa tatu Saa 9:00 hapo hapo Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NI YANGA NA AZAM, SIMBA NA SINGIDA NGAO YA JAMII TANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top