• HABARI MPYA

  Tuesday, March 07, 2023

  SIMBA SC YABISHA HODI ROBO FAINALI LIGI YA MABINGWA


  BAO la kiungo Mzambia, Clatous Chama dakika ya 45 limeipa Simba SC ushindi wa 1-0 dhidi ya Vipers ya Uganda katika mchezo wa Kundi C Ligi ya Mabingwa Afrika leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Ushindi huo unaifanya Simba SC ifikishe pointi sita na kusogea nafasi ya pili, nyuma ya Raja Casablanca yenye pointi 12 na mbele ya Horoya yenye pointi nne na Vipers pointi moja baada ya wote kucheza mechi nne.
  Ushindi huo unaweka hai matumaini ya Simba SC kwenda Robo Fainali ya michuano hiyo kuelekea mechi mbili za mwisho dhidi ya Horoya Dar es Salaam Machi 18 na Raja Casablanca nchini Morocco Machi 31.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YABISHA HODI ROBO FAINALI LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top