• HABARI MPYA

  Wednesday, March 01, 2023

  FRIENDS OF TULIA TRUST YATOLEWA NA ESPANYOL


  TIMU ya Friends of Tulia trust wayaaga Mashindano rasmi kwa upande wa Wanawake na  Wanaume kutokana na kipigo kikali kutoka timu ya Espanyol.                                   
  Sodo upande wa wanawake Friends of tulia walipata kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya  Espanyol, katika sodo wanaume friends of Tulia Trust walibamizwa mabao 2-0 na Espanyol.                  
  Akizungumza Afisa Habari wa Kampuni ya Betika Juvenalius Rugambwa, alisema kuwa Mchezo huo wa Sodo 4 Climate  una lenga zaidi kuhamasisha Mazingira kuwekwa safi hususani maeneo ya Fukwe za Bahari.
  "Lengo la Mchezo wa Sodo 4 Climate ni kukumbusha jamii kufanya usafi na kutunza Mazingira ya Fukwe za bahari ambapo ligi hii inaendelea kufanyika maeneo ya Fukwe hizi za Coco Beach. 
  Rugambwa ameeleza kuwa Mchezo huo  kati ya Friends of Tulia trust dhidi ya Espanyol zilihusisha upande wa Timu ya Wanawake na Wanaume. 
  " Sodo upande wa wanawake Friends of tulia waliondolewa kwa kufungwa mabao 2-1 dhidi ya wapinzani wao  Espanyol, na sodo wanaume friends of Tulia Trust walifungwa mabao 2-0 na Espanyol. Hivyo Friends of tulia trust tayari wameaga mashindano rasm Alisemai ".


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: FRIENDS OF TULIA TRUST YATOLEWA NA ESPANYOL Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top