• HABARI MPYA

  Sunday, March 05, 2023

  AZAM FC YAICHAPA MAPINDUZI 2-0 NA KUTINGA ROBO FAINALI ASFC


  WENYEJI, Azam FC wametinga Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Mapinduzi FC ya Mwanza Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. 
  Mabao ya Azam FC leo yamefungwa na Cyprian Kachwele dakika ya 26 na Nathaniel Chilambo dakika ya 72 na sasa wanaungana na mabingwa watetezi, Yanga, Simba, Geita Gold, Ihefu SC, Mtibwa Sugar, Singida Big Stars na Mbeya City kukamilisha idadi ya timu za Robo Fainali ya michuano hiyo.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YAICHAPA MAPINDUZI 2-0 NA KUTINGA ROBO FAINALI ASFC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top