• HABARI MPYA

  Tuesday, August 02, 2022

  SIMBA YASHINDA 2-0 MECHI YA KIRAFIKI MISRI


  TIMU ya Simba imeibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Al-Kholood FC katika mchezo wake wa mwisho wa kirafiki kwenye kambi yake ya mjini Ismailia nchini Misri kujiandaa na msimu mpya. 
  Katika mchezo wa leo nyota ilikuwa ni ya beki wa kushoto, Gardiel Michael ambaye pamoja na kufunga la kwanza, pia akatoa pasi ya bao la pili lililofungwa na Mghana, Augustine Okrah.
  Mechi tatu za awali Simba ilitoa droo ya 1-1 na Ismaili, kabla ya kushinda 6-1 dhidi y Abo Hamad na kuchapwa 2-0 na Haras El Hodoud.
  Kikosi cha Simba kinatarajiwa kurejea nchini kesho tayari kwa tamasha la Simba Day Jumatatu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA YASHINDA 2-0 MECHI YA KIRAFIKI MISRI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top